MWANAMUZIKI Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni aliwachefua waumini wenzake wa dini ya Kiislam baada ya kutinga kwenye Maulidi akiwa amevaa hereni na cheni. Tukio hilo lilijiri maeneo ya Tandale, Dar ambapo mama yake aliyemtambulisha kwa jina la Aunt Shani aliandaa maulidi kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu. Akiwa mmoja wa waalikwa, Diamond alinaswa akiomba dua sambamba na rafiki yake aitwaye Remeo Jones ‘RJ’ huku akiwa amevaa kanzu safi na balaghashia lakini akaharibu kwa kuvaa hereni na cheni. Kitendo hicho kiliwachefua Waislam ambapo baadhi walifikia hatua ya kumchana laivu kuwa, alichokifanya kilikuwa kinyume na Uislam. |
0 comments:
Post a Comment