Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu
anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’
kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo
kwa sababu amelipa mahari. Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande
mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu
wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu
wapenda ngono.
Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi
ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana
nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili
kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo
ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika. Twende
pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Watu
wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa
wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza
wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara. Sababu hizo zinaweza
kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata
anapomuona akiwa mtupu.
Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi
kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile
zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile
kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa
mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena
kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA
Tabia
ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini
na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo
la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa
kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa
wakati gani?
Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa
mara ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila
kujali hadhi yake. Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa
watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile
akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi. Unapokuwa mtu wa
kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako.
Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate
kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha ya tendo
hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya
kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara
unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo
haikutoshi kumaliza tamaa yako. Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa
mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI
Madhara
mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni
pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili. Kama tujuavyo tendo la ndoa
hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili
uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa
nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha. Sambamba na hilo mbegu
za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa
dhaifu.
KUPATA MAGONJWA
Kama tulivyojifunza kuwa watu
wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya
mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo
ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa
kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri
kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na
hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka
ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
Baada ya kungalia madhara
hayo machache ni vema kwa wapenzi kupunguza kiwango cha kufanya mapenzi
ili kuifanya miili iwe na uvumilivu unaoweza kumsaidia mtu kukaa kwa
muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake hata kama atakuwa amesafiri mbali
naye kimasomo, kikazi au kibiashara.
Originally posted at Jamii Forums, na MziziMkavu
Originally posted at Jamii Forums, na MziziMkavu
0 comments:
Post a Comment