Mastaa
mbalimbali nchini wameungana na wananchi wengine wa jijini Dar es
Salaam kuombeleza vifo vya watu ambao bado idadi yao kamili
haijajulikana waliopoteza maisha leo asubuhi baada ya jengo lenye
ghorofa takriban 15 kuanguka katika ya jiji hilo.
Jengo hilo lilikuwa likiendelea kujengwa na taarifa za awali zinadai
kuwa karibu watu 60 wanahofiwa kupoteza maisha na shughuli za uokoaji na
kuondoa vifusi ikiendelea.
Haya ni maoni ya baadhi ya mastaa na viongozi wa Tanzania walioguswa na tukio hilo:
Rais Jakaya Kikwete
Dua zangu kwa Watanzania wenzetu waliokumbwa na maafa ya kuanguka kwa
jengo eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam asubuhi yao leo. Undugu
na umoja usiojali tofauti yoyote unaojionyesha katika shughuli za
uokoaji zinazoendelea ni jambo la faraja na la kutia moyo sana.
Mwana FA
Sio mara ya kwanza,hatujifunzi kitu aunty..uzembe wa mijitu mipuuzi unaangamiza maisha ya watu..na bado wanajenga.
Ben Pol
My heart goes out to all those who have lost their loved ones in the
fallen building in the City Centre. So so sad. #Inasikitishasana.
Salama A. Jabir
Mwenyezi Awalaze Pema Walopoteza Maisha Leo Kwenye Jengo Lilodondoka…Matumaini Yangu Tumejifunza Kitu. Insha’Allah Kheri.
Joseph Haule
Haya majengo yanayoota mjini kama UYOGA inabidi yaangaliwe sana ubora
wake, la sivyo tutazidi kupoteza Ndugu zetu kila Kukicha! POLENI WOTE.
Grace Matata
Now we got buildings crumbling kama utani. Hii nchi, mweeeee…. Dah,
hapa kila jengo ntakaloingia ntakuwa najiuliza mara mbili mbili. Kazi
kweli kweli ndugu yangu.
Allan Lucky
Kuna jengo lipo katikati ya jiji kabisa, nina wasi wasi ipo siku
litaporomoka. Mi sio mkandarasi, but naliogopa! Watu wa viwango mko
wapi?
Lady JayDee
Hivi hizi habari huwa zinatokaje, Mara ghorofa 17, 12, 16 mara 15?
Tuelewe lipi? Hakuna mwenye uhakika ina maana? Mmhh!! Poleni wafiwa.
Arnold Kayanda
Nawatakia kupona haraka walioumia,Mungu awarehemu waliofariki! Natoa pongezi kwa wote wanaoshiriki katika uokoaji!
Vanessa Mdee
Saddened by the news of this sudden collapse of a building in the
city centre. Thoughts n prayers to the families who’ve lost loved ones.
Tayana S Tibenda
Inasikitisha sana tamaa ya hela unaua watanzania?!!?? Huyu mwenye
hili gorofa lililoangua leo posta afungwe..mxxiiiiiiii kabisa. More sad
watoto maskini waliopoteza maisha yao!
Maua Sama
RIp to those hu died in the accident ..!! NA Mungu awaponye wale majeruhi..Ameen!
Bernard Membe
Nimesikitishwa na taarifa za ajali na vifo kutokana na kuanguka kwa jengo.Natoa pole kwa wafiwa na majeruhi,uongozi wa mkoa na @JerrySilaa
Nimesikitishwa na taarifa za ajali na vifo kutokana na kuanguka kwa jengo.Natoa pole kwa wafiwa na majeruhi,uongozi wa mkoa na @JerrySilaa
January Makamba
My TL on collapsed building: only few are praying for the victims.
Only one inquired about contributing to rescue efforts. Blame dominates.
Mwezi uliopita jengo lenye ghorofa nne jijini Dar es Salaam
lilianguka na kusababisha kifo cha mtoto mmoja aliyekuwa na umri kati ya
mika 10 hadi 11.
0 comments:
Post a Comment