Ni
ngumu kuamini lakini ni kweli Chidi Benz kampiga mshkaji wake wa siku
nyingi na waliyewahi kushirikiana kwenye ngoma, 120, Albert Mangwea.
Rapper
Chidi Benz, amempiga Cow Bama a,k,a Ngwea nje ya Ambassador Lounge
ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku wa kuamkia leo (usiku wa kuamkia jana
Jumapili). Ugomvi huo ulitokea baada ya Chidi kumzingua Dully alipokua
akiingia, ambapo mwisho wake aliamua kuondoka.endelea kupitia
audifacejackson blog,..
Baada
ya Dully kuondoka, Ngwea aliamua kumuuliza Chidi (ambae mara nyingi
huitana Dogo lao), inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chidi
alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza
Ngwea, inasemekana Ngwea aliamua kukaa kimya lakini Chidi aliendelea
kuongea kwa hasira na kusema “ndio nimemzingua kwani yeye nani” na
kumbadilikia Ngwea ambae pia aliamua kuachana nae na kurudi ndani kwenye
meza aliyokua amekaa na washkaji zake. Haikuishia hapo Chidi amkamfata
kwenye meza hiyo na kuanza kumuongelea mbaya Ngwea, na ndipo Ngwea
akaamua kushuka chini ya jengo kwa nia ya kuondoka.
Watangazaji wa Clouds FM Adam Mchomvu na Dj Fetty wakiwa na Chidi Benz Ambassador Lounge
Akiwa
huko huko chini Chidi alimfata na kumpiga, ikiwa ni pamoja na kumkata
na chupa mkononi,na kupelekwa hospitali ambapo alitibiwa.
Nimeongea
na Ngwea ambae anasema haoni chochote kilichomfanya kupigwa na msanii
huyo. Ngwea kwa sasa yupo katika kituo cha polisi Oystabay kwa ajili ya
kumfungua mashtaka, licha ya kuumizwa pia ni kutokana na vitisho
alivyopewa na Benz.
Kutokana
na kitendo hicho, mashabiki wamemshambulia Chidi kwa matusi ya nguoni
kupitia Twitter na hizi ni miongoni mwa tweets hizo:
@cloudcharles91:
@chidibeenz umeniboa tena umeniboa sana kumzingua mwanangu @ngwair kama
mziki umekushinda kaa pembeni f*la wewe” umepaniki.
@chidibeenz
wanaume rijali atutoboi pua punga ww.. Km unajua pgana, kampge Ney na
@diamondplatnumz uko.. achana na @ngwair mtu wa watu ote!
The
real yunus: @ngwair no beef…mtu wangu wa nguvu malipo ni duniani waache
watoboe pua mwisho wa siku watatoboa maeneo ambayo wakitoboa hata kukaa
shida.
“@cloudcharles91: @chidibeenz we ms***e hata kama @ngwair kakuzingua ndo umpige umeniboa sana we boya k*** m*ko”
“Hizo bangi za ukubwani broh,, huoni km ni risk kumpiga mtu na chupa?? 2ngempoteza 2naemuhtaji zaidi yako @ChidiBeenz @ngwair.”
“Umeone eh? I swear bange mbaya sana yani nimekushangaa kwa hili @chidibeenz @ngwair pole ngwair my bro get well soon mwaya.”
Kwa upande wake Chidi Benz alioneshwa kusikitishwa na kitendo cha Ngwair kuretweet matusi yanayomwendea yeye.
‘Siamini
kama albert una retweet hii kitu, don’t pretend..hawa. Watu ni watu tuu
na watabaki watuu tuuu.na maneno.We unatukana now na unafanya iwe ni
kitu, mimi kama unahisi nimekosea mimi Naomba nisamehe kama
ulivyowasamehe wengine,” alitweet Chidi.
Alimwambiwa
pia Fetty, “kitu nachojua pale ni ofisini kwenu hamtakua mmependa picha
ya ugomvi, mimi na ngwea hatuna ubaya naomba tusameheane mnisamehe.”
“Mashabiki
msisahau na sisi ni mashabiki wa vitu vingine na tuna maisha mengine,
na usijudge maisha ya usiku mimi nikosee au wewe au yeye, “aliongea
Chidi.
Lakini Ngwair, ameonesha kutopanic na kutweet vitu vya busara na kwamba ameliacha tukio hilo lipite.
“Am never weak but Strong Enough to Let it Go,” ametweet.
“I don’t know how to fight it’s not my art I rap best.”
“Only
You! If you are right then there is no need to get angry, And if you
are wrong then you don’t have any right to get angry.”
“Stay away from Anger it hurts.”
0 comments:
Post a Comment