Kwa ufupi
Msanii anayetafuta mafanikio kwa kasi, Wema Sepetu
amesema kuwa haoni sababu ya watu kutishiana maisha hasa kwa kipindi
hiki ambacho maisha yapo juu.
Wema alisema hayo kufuatia hivi karibuni
kutishiwa maisha na watu asiowafahamu na kulazimika kuongeza ulinzi
nyumbani kwake na kila anapokuwa anatoka.
Alisema maisha ni magumu na kila mmoja anatakiwa
afanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo, badala yake watu wanaanza
kutishiana maisha.
"Nawashangaa watu wanaoendelea kuwafuatafuata
wengine wanapata wapi ujasiri huo na hali ya maisha ilivyo ngumu na
kuhitaji muda mwingi wa kufanya kazi ili kujikwamua,"alishangaa Wema.
Aidha, aliongeza kuwa hana adui wala mtu ambaye
anamdai au kitu kama hicho hivyo watu wanaomtumia mesaji za vitisho
anahisi wana chuki binafsi na si kingine.
0 comments:
Post a Comment