Masao Okawa ni bibi mwenye umri wa miaka 114, ambapo jumanne ya wiki ijayo atakuwa anafikisha
miaka 115, na tayari kitabu cha Guiness World Records wamemtaja kama mwanamke mzee
kuliko wote duniani pichani anaonekana akiwa na mjukuu wake wa kike na kitukuu chake.
Masao ambae alizaliwa mwaka 1898, amesema siri ya yeye kuishi muda wote huo, si tu
kwamba anakula kitu chochote, bali chochote lakini cha kijapani tu na si vingine.
Wajapani wanapenda kula mbogamboga na samaki na kuepuka kula vyakula vya mafuta
ukilinganisha na nchi zingine. Pia mwanaume mwenye umri mkubwa ni Mjapan
jina lake ni Jiroemon Kimura anamiaka 115.
|
0 comments:
Post a Comment