Akiongea na East Africa Radio leo, Shetta amesema japo bado jina
halijawa rasmi, amefikiria kuiita kampuni yake Owkey Music Group na bado
yeye na menejimenti nzima wanalijadili jina hilo.
Hata hivyo amesema tayari kampuni yake imeshamchukua msanii mmoja
aitwaye Rumi ambaye wimbo wake uitwao Kosa utatambulishwa Jumamosi hii.
Ameongeza kuwa baada ya Rumi wapo wasanii watatu watakaosainishwa kwenye
kampuni hiyo pia.
0 comments:
Post a Comment