KIUNGO
Jack Wilshere aliwasili katika Uwanja wa mazoezi wa Arsenal jana akiwa
na gari la hatari aina ya Ferrari ili kufanana na mchezaji mwenzake,
Theo Walcott.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 21 amechukua aina ile ile ya gari Kitaliano
kama alivyofanya Walcott wiki iliyopita katika kipindi ambacho Arsenal
inajiandaa vyema na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa Kaskazini mwa London
kwenye Uwanja wao wa Colney.
The Gunners watasafiri Kaskazini mwa London kesho kwenda kupambana na wapinzani wao wakuu, Tottenham.
Breki ya kwanza Tottenham: Jack Wilshere akiwa na gari lake aina ya Ferrari katika Uwanja wa mazoezi wa Arsenal, Colney jana
Mchezaji mwenzake Wilshere, Theo Walcott akiwa katika Ferrari kama ile ile
Maandalizi: Walcott na Wilshere wakijifua na wenzao
0 comments:
Post a Comment