Jamal
Sambeke mtoto wa marehemu akifunga jeneza la baba yake mara baada ya
watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho nyumbani kwake njiro Themi
Mkoani Arusha
Waombolezaji wakibeba jeneza la Bilionea Babu na kuweka kwenye gari maalumu tayari kwa safari kuelekea Moshi kwa mazishi
Watu wakitoa heshima za mwisho
Watoto wa marehemu Sia na Getrude waliovalia nguo nyeupe
Jamal akifunga jeneza la marehemu Babu Sambeke
Jaji Aisha nyerere msibani pamoja na mkurugenzi wa kibo palace Vicent Laswai
Baadhi ya magari ya kifahari yaliyofika katika msiba huo
Mkurugenzi wa hoteli ya Kibo Palace Vicent Laswai akizungumza msibani mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho
Waombolezaji
Mamia
ya vigogo pamoja na watu mbalimbali wafurika nyumbabi kwa marehemu
Bilionea “Babu Sambeke”Ernest Sambeke eneo la njiro jijini Arusha
kuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake eneo la
Karanga mjini Moshi huku msiba huo ukiwa tofauti na misiba mingine
iliyozoekeaka hapa Nchini
Marehemu,Sambeke
alifariki hivi karibuni katika ajali ya ndege aliyokuwa akiiendesha na
pia mmiliki wa ndege hiyo ambapo ilianguka katika eneo la Kisongo na
kusababisha kifo chake Mkoani Arusha
Shughuli
za kuaga mwili wa marehu zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku
mwili huo ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa
kuelekea nyumbani kwake Moshi kwaaajili ya mazishi
Taratibu
za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku
wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka hapa
Arusha na Moshi walionekana kutawala msiba huo.
Katika
zoezi hilo la kuaga mwili wa mareheu Padri Florentine Mallya ambaye ni
mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu na baada ya
kumaliza alitoa fursa kwa watu mbalimbali kupita mbele ya jeneza
kwaajili ya kuaga mwili
Ndani
ya jeneza marehemu alivalishwa nguo zake za kirubani huku ,baadhi ya
wanajeshi kutoka jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walionekana jana
katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadhi yao walikuwa
wamevalia sare za jeshi hilo
Hatahivyo,baadhi ya watu walionekana katika hali ya kawaida huku watoto wakionekana na nyuso za huzuni mda wote
Tofauti
na misiba mingine nchini watu mbalimbali walipata fursa ya kupata
chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia vikiwemo vinywaji aina
ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana
wakijihudumia zaidi vinywaji vya bavariaMagari ya kifahari yalionekana kutawala msiba huo huku barabara ya njiro ikionekana kuwa na msongamano kubwa iliyosababishwa na zoezi hilo la uwagaji wa mwili
Marehemu aliacha watoto watatu ambao ni Sia,Jamal,Getruda
JAMII BLOG
0 comments:
Post a Comment