Uongeaji
ni sanaa pia ambapo kuna wale waliojaaliwa uwezo wa kuongea kwa
mbwembwe zaidi na kuwa kivutio kwa wanaosikiliza. Hawa ni wasanii 10
tunaoamini kuwa huongea kwa mbwembwe zaidi wahojiwapo redioni ama kwenye
TV.
1. Godzilla
Kama haumfahamu Godzilla a.k.a Zizi na hujawahi kumsikia popote,
ukifungulia redio na ukakuta anahojiwa unaweza kuhisi ni mnyamwezi
fulani aliyekaa Marekani kwa muda mrefu sana na Kiswahili kimeanza
kumtoka kichwani. Tangu aanze muziki, Zilla amekuwa akifuata nyendo
nyingi za 50 Cent hasa katika kurap na kuongea. Mara nyingi kwenye
interview hutupia swag kama za 50 na kwa hakika hakuna anayemfikia.
2. TID
Khalid Mohamed aka Top in Dar huongea kwa kujiamini na dharau kiasi
ndani yake (ndivyo alivyo). Katika interview hupenda kuchanganya
Kiingereza mara kwa mara ambacho anakimudu poa pia. Mfano mzuri ni
kwenye U Heard ya juzi kati ya XXL, Clouds FM kuhusiana na kukwaruzana kwake
na Salama Jabir. Mwishoni mtangazaji wa show hiyo Soudy Brown alimuuliza
TID anafanya nini maskani, na TID kujibu, “Nipo naangalia tambala moja
hivi kwenye 3D kwahiyo I need a lot of attention, I am very sorry can
you hang up for me!!”
3. Mr Blue
3. Mr Blue
Blue amepunguza tu mbwembwe siku hizi lakini kama ingekuwa enzi zile,
Godzilla asingefua dafu. Blue ni tozi kitambo na ndiye mhasisi wa
utamkaji wa maneno ya Kiswahili kwa ladha ya kimombo kwa mfano kabisa
itamkwe, kabaisa kitu kilichofanya kuzaliwa kwa aka yake Kabayser.
4. Fid Q
Fid aka Ngosha si mkali tu wa mashairi yenye swagga za moto bali pia
hata uongeaji wake. Pamoja na kwamba anatokea Mwanza ambako Kiswahili
cha huko kimeathiriwa na kisukuma, Fid huongea kama kashuka jana kutoka
states. Uongeaji wake akiwa redioni utadhani ana kigugumizi fulani kumbe
ndio swag ziko on. Izingatiwe pia kuwa The Top of Rap’s elite ni
profesa wa Kitaalojia.
5. P-Funk
5. P-Funk
Majani ni muongoezaji mzuri sana redioni. Background yake ya elimu na
kutembea sehemu kadhaa duniani, kumemfanya asound kama Mmarekani
aongeapo kimombo.
6. Shetta
Shetta aka Bonge la Bwana naye yumo. Anapokuwa akiongea redioni huwa
haoni hatari kutupia maneno kadhaa ya kimombo kushtua kidogo.
7. Q Chilla
Chilla ana uongeaji wa taratibu lakini wenye mbwembwe za hapa na pale hasa za kuchomekea viingereza.
8. Izzo B
8. Izzo B
Uvaaji wa Izzo na uongeaji wake vinaenda sawa. Izzo ni bling blinger
na hewani anapokuwa anahojiwa, hit-maker huyo wa Riz-one hutupia swagga
kibao na kama anahojiwa na mtangazaji mbovu si ajabu yeye ndio akasound
kama mtangazaji wa show, ana vocal kali.
9. Quick Rocka
Quick aka Switcher kama anavyojiita, ni rapper anayeswitch swag kama
kinyonga anavyobadili rangi yake. Kama Izzo B, yeye pia ana sauti ya
mamlaka hewani.
10. Mo Rocka
Sijui nini kilitokea kwa rapper huyu mtanashati lakini kwa speed
aliyokuja nayo kama angekaza, angekuwa mbali. Wakati anaanza kupata
umaarufu wengi walikuwa wakimfananisha na Kabayser hasa kwa jinsi
anavyorap na hata uongeaji wake kwenye redio.
0 comments:
Post a Comment