kama
umekua ukiwafatilia hawa mastaa wawili, stori kwamba hawapatani toka
Ommy Dimpoz alipoondoka Top Band itakua sio mpya kwako.
Ommy ameripotiwa na baadhi ya
vyombo vya habari kwa muda mrefu kutokua na uhusiano mzuri na T.I.D toka
alipotoka kwenye hiyo band.
Baada ya hayo yote, jana April 5
2013 T.I.D akiwa Maisha Club sehemu ya V.I.P alimuita Ommy Dimpoz na
kupiga picha ya pamoja kabla ya kuongea na chanzo kimoja wapo cha habari na kufuta sumu iliyoenezwa kwenye headlines kwa kipindi kirefu.
Kwenye interview hiyo ambayo
itasikika pia kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM jumatatu April 8 2013, T.I.D
amesema “watu wengi wananiona mimi ni Mkorofi lakini niko tofauti sana
na wanavyofikiri, sikuwahi kuwa na ugomvi na Ommy, nimekaa nae kwa miaka
minne….. taarifa za beef ni za watu tu walioamua kuniharibia tu lakini
niko poa na Ommy”
Toka hizo stori zote
zimeripotiwa hatukuwahi kuona wawili hawa wakiwa kwenye furaha na picha
ya pamoja kama hivi kwa zaidi ya mwaka mmoja, pia alichokisema T.I.D
hakimaanishi Ommy amerudi TOP BAND, kila mtu anaendelea na kazi zake.
Unaweza kuwa karibu zaidi na millardayo.com kwa kujiunga kwenye theHOODinfotainment.blogspot.com ili kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata Breaking News mbalimbali muda mfupi tu zinapotokea.
chanzo: millard ayo
0 comments:
Post a Comment