Baada ya taarifa za uhakika
kuripotiwa kwamba Rais wa Venezuela Hugo Chavez amefariki dunia, Rais
Barack Obama wa Marekani amesema nchi yake imehamasika kuanza mazungumzo
ya uhusiano mpya wa nchi hizo mbili.
Rais Hugo Chavez amefariki
akiwa na umri wa miaka 58 akisumbuliwa na kansa ambapo taarifa yake
ilitangazwa usiku wa kuamkia march 6 2013, alietangaza ni makamu wa Rais
Nicolas Maduro ambae sekunde 40 baada ya kuanza kuzungumzia kifo hicho
alishindwa kuzuia hisia zake na kulazimika kuwa kimya kwa muda kutokana
na machungu.
0 comments:
Post a Comment