MASTAA wakali
wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walifunga mtaa na kuanza
kukata mauno kinomanoma na kusababisha umati wa watu
uwazunguke.
Wema Sepetu
na Aunt Ezekiel wakikata mauno.
Mpango mzima
ulitokea hivi karibuni katika arobaini ya mtoto wa dada yake Wema iliyofanyika
Sinza Kwa - Remmy, jijini Dar ambapo Aunt pamoja na baadhi ya wasanii walifika
kusherehekea sherehe hiyo ya kumtoa mtoto.
Awali, Wema
alionekana akimtunza fedha pamoja na mikufu ya dhahabu yenye thamani kubwa na
ilipoisha sherehe ya maulid ndipo mastaa hao waliwasha muziki na kuanza
kulisakata rumba.
“Sisi
tumecheza tumefurahi tu hawa waliofunga mtaa kututazama watakuwa wanataka kuona
mavituzi yetu,” alisema Wema.
0 comments:
Post a Comment