Huenda mliwahi kusikia mkasa uliompata mmojawapo wa viongozi wa ngazi za juu kabisa katika serikali ya nchi ya Liberia iliyoko huko Afrika Magharibi.
Huyu
ndo ndo Bwana Mkubwa Willie Knuckles aliyekuwa waziri wa mambo ya
rais(Minister of Presidential Affairs) huko Liberia ambaye alilazimika
kujiuzulu baada ya picha zake zilizokuwa zikimwonyesha akifanya tendo la
ngono na wanawake wawili kusambazwa kwenye mtandao.
Kwakweli bado
haijaeleweka hasa walioamua kumsambaza mtandaoni walikuwa na lengo gani
naye zaidi ya kumdharirisha na kumfedhehesha namna hii.
Ilikuwa
ni aibu kubwa sana kwake na kwa familia yake,serikali ambayo yeye
alikuwa ni mhimili wake na hata wananchi wote wa Liberia (picha hii
nimekata "croping" makusudi kulinda maadili ya mtanzania,lakini shughuli
iliyokuwa inafanyika nafikiri inaonekana).
Haijaelezwa vizuri
kuwa ndoa yake ambayo ilikuwa na takribani miaka 37 mpaka anakutwa na
maswahibu haya iliishilia vipi,vyovyote ilivyokuwa Bwana mkubwa Knucles
atakuwa alivuna alichokuwa amekipanda.
Hapa Tanzania kina" Willie
Knucles" wako wengi sana,wababa wanaopenda kutumia nyadhifa zao na
mapesa yao ambayo kwao huona ni vijisenti kwa kuwarubuni mabinti tena
wadogowadogo na kufanya nao ngono.
Binafsi huwa nashikwa na hasira
sana ninapoona binti mdogo anatoka na M'baba anayefaa kuwa Baba yake
Mzazi ni mambo ambayo yapo sana katika jamii yetu hata kijijini kwangu
ninapoishi Kiluvya wazee wa type hii wapo sana ndo maana kasi ya
kusambaa kwa virusi hatari vya Ukimwi inazidi kukua kila kukicha,in
which way tunaweza kupona ikiwa mambo haya yataachiwa yaendelee ku'apply
katika jamii zetu?
Lakini na nyie ma'binti hivi na lazima kweli
m'date na Wababa wanaolingana na Wazazi wenu?(hili nalo ni swali
ninaloliulizaga sana... majibu ambayo nimekuwa nikiyapata yamekuwa
hayaniridhishi hata kidogo,eti utamsikia demu anasema eti Vijana
wasumbufu sana....nyie mmelogwa?)
Blog hii inatoa
tahadhari,yaliyompata Bwana Willie Knucles iwe ni fundisho kwa wote
wenye tabia hii,siku hizi technolojia imekua sana,unaweza kudhalilishwa
dunia nzima katika dakika chache tu,kuna simu za kichina siku hizi zina
Camera 4,4 (mbele nyuma na pande zote 2)
Shauri zenu mnaweza kujikuta kwenye "The World of Anselm" mkabaki kunisaka kwa udi na uvumba.
chanzo:hans4real.blogspot.com
chanzo:hans4real.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment