Diamond akiwa mbele ya Prado yake siku alipoamua kuitangaza kwenye media june 2012. |
Kupitia post hii the HOOD infotainment
inakujulisha kwamba mwimbaji staa ambae ndio mwimbaji Mtanzania
alieongoza kwa kuandikwa sana kwenye internet mwaka 2012, Diamond
Platnums ametangaza mpango wa kununua gari jingine.
Tofauti na Prado aliyoinunua
june 2012, Diamond hajataka kutaja ni aina gani ya gari aliloliagiza
sasa hivi lakini kakubali kwamba kaliagiza Japan na litakua la gharama
ya juu kuliko Prado.
Ukiachia mbali hilo gari
analoliagiza, Diamond amekiri pia kwamba amemaliza kuijenga nyumba yenye
gharama ya milioni mia mbili sitini ambayo ameijenga maalum kwa ajili
ya mama yake mzazi.
Diamond ambae amekua akiandamwa
na maneno maneno ambayo anaamini wanaoyasambaza ni wasiompenda amesema
“mimi nikimtanguliza Mwenyenzi Mungu mbele ata mtu atake kunifanya kitu
gani haweziii mpaka aandike Mwenyenzi Mungu mwenyewe, ndio maana wao
kila wakipiga vita… mimi nazidi kuwa maarufu, nazidi kuwa na hela… sasa
hivi nabadilisha Prado nanunua gari jingine….. jamani mtaiona”
0 comments:
Post a Comment