Hivi
karibuni Diamond Platnumz alilazimika kuahirisha ziara yake ya barani
Ulaya baada ya waandaaji kushindwa kukamilisha kumlipa hela yake ya
advance katika muda muafaka.
Inadaiwa kuwa katika ziara hiyo Diamond alitakiwa kulipwa dola 50,000
ambazo ni takriban shilingi milioni 80 za Kitanzania na ameithibitishia the HOOD infotainment kuwa ni kweli japo kuna taarifa kuwa kiasi hicho alikikataa.
Ameiambia the HOOD infotainment kuwa ziara hiyo itafanyika mwezi ujao ambapo baada
ya ziara hiyo atarudi nyumbani na kisha kwenda tena kwaajili ya
nyingine. Kutokana na makubaliano mapya ya ziara hiyo kuna uwezekano wa
ziara hiyo ya kwanza kumuingizia karibu shilingi milioni 100 ama zaidi.
Jumamosi hii Diamond alilazimika kutumia website yake kutoa taarifa ya kuahirisha kwa ziara hiyo.
“Kutokana na kampuni ya United Events Ltd Tilburg-The Netherlands kwa
upande mwingine kama promoter kushindwa kutimiza baadhi ya mahitaji
ikiwemo kushindwa kulipa pesa ya show ambayo ilitakiwa ifanyike
Jugenhause Ostend mjini Stuttgart/Germany 09/03/2013 na zingine kama
East African Night ambayo ilitakiwa ifanyike mjini Rotterdam/Holland
tarehe 15/03/2013 na kadhalika, mimi na team yangu nzima ya wasafi
hatutoweza kuhudhuria kwenye events hizo,” alisema.
“Nilikuwa nikipata maswali mengi sana toka kwa mashabiki zangu
mbalimbali wakiniuliza kuhusiana na ujio wangu wa nchi hizo za EUROPE
lakini siku zote nilikua kimya sikuweza kujibu wala kuzungumza chochote
na wadau wangu kutokana na kutokuwa na uhakika wa tour hiyo.”
0 comments:
Post a Comment