Na Mwandishi Wetu
KWA
muda mrefu, zilisikika sauti za kupiga vita makundi ya wanawake
yaliyosifika kwa kucheza utupu kwa kulowanisha khanga maji maarufu kama
Khanga Moko Ndembendembe lakini sasa imeibuka nyingine, inayoitwa Fulana
au Tisheti Ndembendembe, fahari ya kusini inabumburua.Uchunguzi
wetu wa miezi kadhaa tangu mwaka jana ulibaini kwamba tayari staili
hiyo ya uchezaji wa muziki wa mwambao kwa kulowanisha tisheti laini
nyeupe kwa maji na kusababisha chuchu kuonekana sawia, inazidi kushika
kasi kama moto wa kifuu Bongo.
Ilibainika kuwa staili hiyo ambayo ilianzia Pwani ya Kenya, sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini hasa kwenye ngoma maarufu za ‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana. |
Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa.
Mamlaka na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa nguvu zote kwani huo ni mwanzo mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania na ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
0 comments:
Post a Comment