Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Niwe Nawe Milele,
Rehema Chalamila aka Ray C anatarajia kurejea tena kwa kishindo kwenye
muziki. Ray C anatarajia kuonekana rasmi kwenye shughuli za kawaida na
za muziki wiki ijayo. Tumezungumza naye leo kuhusu maisha yake sasa
hivi, alivyobadilika na ujio wake mpya kimuziki.
Kuhusu kama yupo tayari kufanya muziki
I am more than ready, wakati nipo huku nilikuwa naandika andika nina
nyimbo kama tatu nne hivi kali sana. Sema ningependa tu kuwaambia
mashabiki wawe na uvumilivu kwasababu wameniombea sana na wengi kwenye
Instagram, Facebook walikuwa ‘when are you coming back, we miss you’
vitu kama hivyo. Na mimi ningependa kuwaambia tu kwamba wiki ijayo ndio
narudi rasmi, kwa wale ambao walikuwa na wasiwasi, ‘where is Ray C, Ray C
atarudi tena kwenye muziki’ na vitu kama hivyo. Tutaanza kuingia studio
next week, kila kitu kitaanza next week. Lakini kama nyimbo kuandika na
kila kitu vyote viko tayari.
Kuhusu aina ya nyimbo atakazokuwa akiimba zaidi
Nafikiri sasa hivi ntabase kwenye maisha zaidi. Nafikiri watu
wanahitaji kujua mambo ya maisha zaidi. Unajua mimi tangu mwanzo
nilikuwa naimba mapenzi, ofcourse nyimbo za mapenzi zitakuwepo sema
ntabase zaidi kwenye mambo ya maisha.
Kuhusu mabadiliko aliyonayo sasa
Ray C ni kibonge sasa hivi, Ray C amenenepa kidogo. Najua mashabiki
wakiangalia kwenye Instagram wanasema ‘dada vipi bana’ lakini najua
njiani huko ntapunguapungua. Lakini Ray C wa sasa hivi sio kale
kembambaa kale mlikokazoea kale. Sasa hivi Ray C kidogo amevuta shavu
kwahiyo wakiniona wasishangae. Halafu pia kwa sauti niko fit sana. Yaani
all along nilikuwa nafanya zaidi mazoezi kwasababu nimepata sana muda
wa kupumzika, mazoezi ya kuimba, yaani nimeona nipo tofauti na zamani.
Kuhusu sababu za kunenepa
Si unajua tena maisha mazuri, kula kula vizuri, kutulia kwa muda bila
kufanya kazi ndio maana nikafutuka kidogo lakini ntafanya mazoezi,
ntapungua si unajua lazima nipungue kidogo ili niweze kuimiliki
stage,vile nilivyokuwa zamani au better zaidi.
Kuhusu wasanii wapya anaowasikiliza
Namsikiliza sana ambaye namkubali ni mdogo wangu Recho. I think
kwasababu muziki wake kidogo umefanana na wangu kwahiyo napenda ladha
yake halafu kuna Diamond pia namsikiliza, ni msanii ambaye anafanya
vizuri sasa hivi kwahiyo namsikiliza pia kuna kitu gani hapo watu
wanakipendea zaidi niibeibe maideas hapo nifanye kazi nzuri.
Kuhusu alivyojiskia baada ya kusikia nyimbo za Recho
Recho mimi namjua kabla hajatoka na alikuwa anapenda sana nyimbo
zangu, alikuwa anasikiliza sana nyimbo zangu. Mara ya kwanza nimemuona
alikuja akaniambia ‘dada Rehema naomba nikuimbie wimbo mmoja’ akaniimbia
‘Umenikataa Bila Sababu’, akaniimbia nyimbo kama tatu hivi. Kwahiyo
namjua kabla hata hajaingia studio. Kwahiyo nilikuwa najua kabisa
nimemuinfluence kiasi gani.
CHANZO: BONGO 5
Friday, August 2, 2013
Ray C afunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ujio wake mpya
9:20 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment