KUSOTA Gereza la Segerea, Dar kwa madai ya
kumuua bila kukusudia aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba
kumemfanya mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kubadilisha mtindo wa maisha na
kuishangaza jamii,
Lulu wa sasa si yule wa zamani ambapo
inahabarishwa kuwa ameachana na tabia za kwenda kujiachia klabu, kulewa hadi
kupitiliza, kulala kwenye mageto ambapo sasa amekuwa ni mtu wa kumtukuza Mungu,
muumba wa mbingu na nchi.
HULALA SAA 3:30 usiku
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Lulu (aliomba
jina lisitajwe), tangu staa huyo atoke jela amebadilika tabia, ameacha anasa za
dunia hali inayomfanya wakati mwingine alale saa 3:30 usiku au saa
4:00.
ANASOMA BIBLIA KILA SIKU
“Yaani Lulu amebadilika sana tangu alipotoka
jela, anasoma Biblia kila siku, zamani hakuwa hivyo. Kuna watu wanasema bado
anapenda kwenda kujiachia klabu kama zamani, si kweli jamani,” kilisema chanzo
hicho.
JUMAPILI AKIKOSA KANISANI ANAKOSA
AMANI
Imezidi kumiminishwa kwamba Lulu amejenga
tabia ya kutokosa kwenda kanisani kila Jumapili. Japokuwa zamani alikuwa akienda
lakini kwa sasa ni kama dawa, akikosa anashinda akiwa hana amani.
HAENDI MAGETO YA WENZAKE
Habari zilisema kuwa kwa sasa, Lulu amekuwa
mzito kunyanyua miguu yake kwenda kwenye mageto ya wenzake kama ilivyokuwa
zamani.
“Zamani Lulu alikuwa anaweza kulala nje ya
kwao, hasa kwenye mageto ya rafiki zake hata wiki moja na mama yake (Lucresia
Karugila) asijue alipo, siku hizi ameacha. Kama atalala nje, mama yake anajua ni
wapi na lazima itakuwa sehemu yenye usalama kwa mwanaye.
NINI KILICHOMBADILISHA LULU?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Lulu
amebadilishwa tabia na mama Kanumba (Flora Mtegoa) ikidaiwa kuwa mara baada ya
kutoka jela, alikwenda nyumbani kwa mama huyo, Mbezi, Dar na kumuomba msamaha
ambapo mama Kanumba kama binadamu alimsamehe kwa moyo mmoja, jambo ambalo Lulu
hakulitarajia.
MAMA KANUMBA ANASEMAJE?
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari
wetu alimtafuta mama Kanumba ili kueleza ukweli kuhusu mabadiliko ya Lulu ambapo
alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa historia aliyokuwa nayo Lulu huko nyuma
ni kweli amebadilika na mabadiliko haya yametokana na mimi.
KUMBE ALIPOTOKA JELA ALIPIGA HODI KWA MAMA
KANUMBA!
“Baada ya kutoka jela tu (akiachiwa kwa
dhamana) Lulu alikuja nyumbani kwangu na kuniomba msamaha kwa
yaliyotokea.
“Niliamua kumsamehe kwa moyo wote, kitu
ambacho hakukitegemea.
“Baada ya msamaha huo, nilimkalisha chini na
kumshauri kuwa aachane na mambo ya dunia. Nilimwambia yote yaliyotokea Mungu
alikuwa na makusudi maalum kwake, ndiyo maana akampitisha kwenye mapito hayo ili
abadilike.
“Namshukuru Mungu, baada ya mazungumzo yale
Lulu aliamua kubadilika kabisa, amekuwa mtu wa kusoma Biblia. Muda mwingi
anautumia kusali. Lulu amekuwa mshauri wangu mkubwa, kila ninapokuwa na jambo
linalonikwaza anatumia maneno ya Biblia kunirudisha sawa, anajua sana maneno ya
Mungu kunishinda hata mimi. Familia zote mbili (na ya mama Lulu) tunamuombea
aendelee hivyohivyo.”
Mama Kanumba hakuishia hapo, alisema kuwa
Lulu amekuwa ni mwanaye na ndiye faraja yake kubwa japokuwa Kanumba hayupo tena
lakini staa huyo anaendelea kumpenda na kumheshimu kama mama yake.
AUTAJA UNDUGU NA MAMA LULU
Mama Kanumba alikwenda mbele zaidi kwa
kusema kuwa kwa sasa yeye, mama Lulu na Lulu mwenyewe wamekuwa ndugu na hiyo
yote inatokana na jinsi msanii huyo alivyomfuata baada ya kutoka
jela.
WASANII BONGO MOVIES HAWAAMINI
Kufuatia mabadiliko hayo, inadaiwa kuwa
baadhi ya wasanii wa filamu za Kibongo wamekuwa hawaamini kama Lulu huyu si yule
wa enzi za Kanumba, huku wengine wakidai baada ya muda mfupi atarejea maishayake
ya zamani.
LULU NAYE
Lulu kwa sasa anadai hataki kuongea na
magazeti, lakini akizungumza kupitia Kipindi cha Take One cha Clouds TV hivi
karibuni, msanii huyo alikiri kubadilika kutokana na maisha aliyoishi
jela.
Alisema kwa sasa amekuwa ni mtu wa kusali na
kusoma Biblia, starehe alizokuwa akiziendekeza zamani ameziacha, jambo ambalo
limeshangaza watu kwenye jamii
0 comments:
Post a Comment