Mkuu
wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza akishuhudia mrundikano wa magodoro
sehemu wanayolala wavulana wa shule ya Mount Zion kwenye moja ya vyumba
vya darasa vilivyotengwa kwa ajili ya kujisitiri.
Vyoo vilivyobananishwa ndani ya bweni pembeni yake kuna masanduku ya nguo ya Wanafunzi.
Hawa
Wanafunzi walifichwa na mwalimu wa shule hiyo baada ya kusikia Mkuu wa
Wilaya anakuja kufanya ukaguzi wa ghadla kwenye hiyo shule.
Wanafunzi
wa kidato cha kwanza waliojificha na mwalimu wao wakirudishwa shuleni,
lengo la kujificha ilikua ni kukwepa kukutwa wamekalia ndoo kwenye
msongamano madarasani.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela akizungumza huku machozi yakimlenga kutokana na
alichokiona shuleni hapo, aliagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi
ya Mkurugenzi wa shule hiyo ya Mount Zion Ilemela.
.
Shule
ya Sekondari ya Mount Zion ina jumla ya vyumba 7 vya madarasa ambavyo
ilisajiliwa navyo kuhudumia wanafunzi 160 lakini sasa hivi wanafunzi
wameongezeka na kufikia 515 ambapo madarasa mengine yana wanafunzi mpaka
119 na wengine wanakalia ndoo badala ya viti.
.
.
Kingine
kilichogundulika ni kwamba Wanafunzi wanaosoma hapa wengi wanatoka
mikoa mbalimbali ambapo huyu mjumbe aliwauliza na wanafunzi kumjibu
Mikoa waliyotajaambayo ni Shinyanga, Mara, Kagera, Dodoma, Mbeya,
Morogoro, Tanga na hata Dar es salaam wapo.
Nje ya Hostel.
Wanalala hapa, tazama jinsi hata walivyoweka vyandarua
.
Ni
ndani ya moja ya vyumba vya wasichana ambacho ndani yake kuna matandiko
haya na masanduku 13 ikimaanisha ndiyo idadi ya wasichana wanaolala
hapa.
Chumba kingine cha Wasichana.
Akiwa
amepakizwa kwenye pikipiki kuelekea zahanati ya jeshi iliyo karibu na
eneo la shule, mwanafunzi huyu aliyekuwa hoi akiumwa na alikutana njiani
na msafara wa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya
Ilemela Amina Masenza ambae aliagiza moja kati ya magari kwenye msafara
wake kumpeleka hospitali.
Aliingizwa humu.
Baada ya mapungufu mengi
kuonekana ikiwa ni pamoja na kukosa mabweni, Idara ya Afya Halmashauri
ya Manispaa ya Ilemela Mwanza imetoa agizo la kisheria kuifungia mara
moja shule ya Sekondari ya Mount Zion kutokana na kukiuka kanuni za
uendeshaji wa shule pamoja na shule hiyo kukithiri kwa uchafu.
Ripoti hii imeandaliwa na mwandishi Albert G Sengo ambae pia ni mmiliki wa gsengo.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment