Bilionea
wa nchini Australia Clive Palmer ametangaza mipango yake ya kujenga
meli pacha ya Titanic lakini hii ikiwa na lifeboats za ziada ili kuwa na
usalama zaidi kuliko ya mwanzo.
Zaidi ya karne baada ya Titanic original ambayo ilidhaniwa kuwa
haitaweza kuzama baharini lakini ikagonga jiwe la barafu la kuzama
kwenye bahari ya Atlantic katika safari yake ya kwanza, Palmer anasema
anadhani muda umefika kumalizia safari hiyo ambayo haikumalizika
kuelekea New York.
“Titanic ilikuwa ni meli ya ndoto. Titanic II ni meli ambayo ndoto
zitakuwa kweli,” alisema Palmer said jijini New York wakati wa uzinduzi
wa mradi huo.
Meli hiyo itakuwa na madaraja yale yale matatu kama meli ya kwanza
iliyotengenezwa mwaka 1912, daraja la kwanza, la pili na la tatu na
abiria hawatakuwa na uwezo wa kuingiliana kwenye madaraja hayo.
Titanic ya pili itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 2,600 na
wafanyakazi 900 na safari itaanzia Southampton hadi New York ifikapo
mwaka 2016 katika safari itakayokuwa kama ile ile ya mwanzo na bila
shaka bila kuzama tena.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mashable, Palmer ameshaanza kupokea ofa za tiketi moja itakayouzwa kwa dola milioni moja.
0 comments:
Post a Comment