Baada ya hili kanisa la Pool of
Siloam Kianga Zanzibar kuchomwa moto saa 9 usiku wa kuamkia february 19
2013, Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo Penuel Elisha amesema sio
rahisi kujua kwa haraka aliyehusika na hilo tukio japokua kumekuwepo na
historia ya mgogoro kati ya kanisa hilo na msikiti uliopo karibu na eneo
hilo.
Namkariri Elisha akisema
“tukio lilivyokua, majira ya saa kumi na dakika 34 nilipigiwa simu na
mchungaji mwenzangu aitwae Israel akaniambia kanisani kwetu
kumeshavamiwa na mlinzi anapigwa mawe, nikachukua hatua ya haraka kuna
mchungaji wetu mgeni ambae ni mkuu wa kanda nikamuamsha nikamwambia
tumeshavamiwa, nilikua na namba ya polisi mmoja wa Mwera ambae
alietusaidia kwenye tukio lililopita la mwaka 2011, nikampigia akapokea
na kuchukua hatua za haraka sana”
Kwenye sentensi nyingine
naendelea kumkariri mchungaji huyu akisema “nakumbuka mwaka 2011
walikuja watu zaidi ya 80 wakiwa na nyundo na sururu wakalibomoa hili
kanisa lakini jana yake uongozi wa Msikiti wa Kianga ulituita kwenye
nyumba ya Sheha wakawa wanadai kwamba tunadai hatimiliki, uhalali wa
kujenga kanisa hapa”
Mlinzi wa kanisa hilo ambae
alikuepo wakati wa tukio amesema “mi nilikua nimekaa nyumba ya kisima
cha kanisa, walivyopita nikatoka kule nikaingia humu ndani badae
wakarudi wakanurishia mawe nikatoka nikakimbia kuwaamsha jamaa kwamba
nimevamiwa, nikampigia mchungaji simu”
Mpaka sasa Jeshi la Polisi
Zanzibar limesema linachunguza chanzo cha huo moto uliounguza sehemu ya
kanisa hilo la POOL OF SILOAM lililopo Kianga nje kidogo ya mji wa
Zanzibar, naibu Mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar Yusuf Ilembo
amesema hilo tukio linahitaji uchunguzi wa kina ili kufahamu waliohusika
ambapo mpaka sasa hakuna aliekamatwa.
0 comments:
Post a Comment