Rapper mkongwe wa kundi linalopewa heshima kama lilitengeneza njia ya
muziki wa kizazi kipya nchini, Kibacha aka KBC da Kwanzanian (wa kwanza
kushoto kwenye picha) amefunguka kuhusiana na sababu anazoona
zimechangia matokeo mabovu ya kidato cha nne ambayo tangu yametangazwa
yamegeuka kuwa gumzo kubwa.
Kibacha amesema,
Bongo flava+hiphop,Bongo movie,Miss Tanzania,Bongo media, kumbi za
starehe,blogs,websites.. wote tunahusika kwa njia moja au nyingine
kuchangia kutoa matokeo mabovu ya mitihani ya secondari 2012, ambapo
67% failed (division zero).
Hawa wanafunzi wote ni mashabiki wako!!.. lawama kubwa ya kwanza ni
kwa mfumo mbovu wa elimu na uliopitwa na wakati.. “very outdated
curriculum” cannot meet 21st century demands.
Wewe entertainer ndio umekuwa role model wa hawa wanafunzi, kuanzia
leo nakuomba ufikirie ni jinsi gani utamsaidia shabiki wako huyo
“mwanafunzi” kuzingatia masomo??
Nyie waandaji wa matamasha ya muziki, wateja wako wengi ni
“wanafunzi”.. wewe mtangazaji wa kipindi maarufu katika redio na tv..
watazamaji wako wengi ni wanafunzi, kuanzia leo fikiria nini mchango
wako katika kuokoa taifa la kesho.
Tusikae na kuiachia goverment na politicians, vijana hawa wanafunzi
hawasikilizi siasa au bunge, wanasikiliza entertainers.. act now!! okoa
jamii.
NA: http://www.bongo5.com
0 comments:
Post a Comment