Kesi ya Uchochezi na Uharibifu
wa mali inayo mkabili Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake leo imeendelea
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam huku Polisi
wakiwa katika doria kali ya kuimarisha ulinzi katika viunga jirani na
Mahakama hiyo ambayo imejizolea umaarufu mkubwa jijini Dar es Salaam na
Tanzania kwa ujumla kwa jinsi inavyo endesha kesi na watu wa aina
mbalimbali kufikishwa katika mahakma hiyo kabla ya baade kesi zao
kuhamia Mahakama Kuu kwa hatua zaidi za kisheria.
Father Kidevu Blog ilikuwepo
kufuatilia matukio ya hapa na pale na zifuatazo ni picha mbali mbali za
tukio hilo na pia kesi hiyo inataraji kuendelea tena Mahakamani hapo
kesho.
Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa katika basi la Magereza tayari kwa kurejeshwa Mahabusu.
Msafara ukianza kutoka Mahakama ya Kisutu
Wafuasi waliokuwa nje wakiimba wakati gari likitoka
Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa Pondawakilifuatilia gari lililombeba kiongozi wao wakati akitoka Mahakama ya Kisutu.
Mkazi wa jiji akipita kando ya
kundi la Askari nje ya Mahakama ya Hakimu Mkzi Kisutu wakati Askari hao
walipo imarisha Ulinzi nbje ya Mahakama hiyo.
Ustaadh huyu alitishiwa na Mbwa akataka kutoka baruti
Wengine zaidi wakitoka Mahakama ya Kisutu
Wakiwapokea na kuwapongeza wenzao wanao tuhumiwa pamoja na Ponda
Kundi la Wafuasi likiwa limejikusanya karibu na Jengo la Sophia House huku Polisi wakiwa kando yao.
Doria barabarani nayo ilikamilika
Ulinzi ulikuwa ni wa Uhakika
Mbwa maalum wa Polisi nao walikuwa kazini hapa wakikata kiu kutokana na jua kali.
Hapa ni Fanya Fujo Uone kilicho mfanya Kanga akose Manyoya shingoni
Kikosi maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKM) nacho kilikuwepo
0 comments:
Post a Comment