Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya
Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga
nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa,
Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo,
Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo.
Kavishe,Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lyaruu,
Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri,
Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka
Marangu na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia,
Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso,
Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo,
Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo
kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao,
inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja
na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada
ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
0 comments:
Post a Comment