Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) |
Najua kama umekua karibu na
media katika siku za karibuni, stori kuhusu uongozi wa bunge la Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania kutangaza mpango wa kutaka bunge lisiwe
linaonekana live kwenye TV utakua umeisikia.
Ni maoni mengi ya Watanzania
yametolewa huku asilimia kubwa ikionekana kupinga huo mpango ambao lengo
lake ni kukwepa kuonekana kwa wabunge wanaovunja kanuni kwa kuropoka na
kufanya vurugu.
Kwenye hii post ni maoni maalum
ya mbunge wa Kawe Halima Mdee ambae namkariri akianza kwa kusema “mmhh…
kwanza ni hoja ya kipuuzi sana na muhimu ikaeleweka kwamba bunge ni
moja kati ya mihimili mitatu ya dola, kinachoonekana kutaka kufanyika ni
muhimili mwingine wa dola kutokutaka umma ujue ukweli kwa kutumia
watumishi wa bunge kwa mantiki ya katibu wa bunge kwa sababu yeye ndio
ametoa hilo tamko ili kuzuia Watanzania wasipate taarifa ambazo tokea
bunge limeanza kurushwa live wamekua wakizipata tofauti na ambavyo
walikua wanapewa hizo taarifa katika mazingira ambayo sio ya wazi”
Kwenye sentensi nyingine Mh
Mdee amesema “nasema hivyo kwa sababu kupitia bunge Watanzania wamejua
mikataba mibovu ya madini, wamejua EPA, wamejua Richmond, Buzwagi,
wamejua jinsi gani fedha zinavyotengwa kwa ajili ya bajeti zimekua
zikitumika vibaya sana kupitia CAG report ambazo zimekua zinajadiliwa
live, Serikali imeona inaumbuka na ikaamua sasa kupitia katibu wa bunge
na kina Lukuvi, tunataja majina ya watu sababu tuna uhakika na
tunachokisema na juzi imeumbuka, sasa wanatafuta statergy ya kuficha”
“Kama mlikua mnafatilia bunge
la juzi mmeona kwamba wameweka sheria kusema kwamba mkaguzi mkuu wa
hesabu za serikali CAG taarifa yake akiisoma haitajadiliwa hadi mwaka
tena mwingine upite waende tena kuedit na kuleta majibu ya uongo, kwa
hiyo kuna mrundikano wa vitu vingi ambavyo Serikali inaona mambo
yakiendelea hivi inawezekana 2015
wakifika watakua wamechoka, sasa wanazuiaje? kwa kuleta vitu vya ajabu
ajabu… kwa hiyo waache wananchi wajue nini kinachoendelea, kuna kanuni
za bunge kama Mbunge anakiuka kanuni” – Halima Mdee
chanzo: millard Ayo
0 comments:
Post a Comment