Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kupitia kitengo cha maudhui
imevifungia matangazo kwa muda wa miezi sita vituo vya radio viwili
nchini kwa kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo ni pamoja na Kwa Neema FM ya Mwanza iliyofungiwa kwa
kuendesha mjadala uliokuwa ukihusiana na watu wa dini gani wenye haki ya
kuchinja wanyama kati ya waislam na wakristu hali iliyosababisha
mgongano wa waumini wa dini hizo.
Kingine ni Imani Radio FM ya mjini Morogoro ambayo imefungiwa kwa
kosa la kupinga zoezi la sensa mwaka jana na kuwashawishi waumini wa
dini ya kiislam wasijiandikishe.
Nayo Clouds FM imepigwa faini kwa kuendesha mjadala kuhusiana na
ushoga pamoja na kuwa na kipengele kwenye kipindi cha Power Breakfast
kiitwacho ‘Jicho la Ng’ombe’ ambacho wametakiwa wakifute kutokana na
kuendeshwa kinyume na maadili.
CHANZO: http// :www.bongo5.com
0 comments:
Post a Comment