Mwili wa Pepetua Maina ukiwa katika shimo la taka.
Issa Mnally na Makongoro Oging'
...Mwili wa Pepetua baada ya kufunikwa.
Taarifa
za kipolisi zilidai kuwa mrembo huyo kabla ya kuchinjwa alipigwa kwani
mkono mmoja wa kushoto ulivunjika na kukutwa na jeraha kubwa katika paji
la uso.
Wakizungumza na Uwazi
kwa tahadhari kubwa kuogopa ushahidi, baadhi ya majirani wa eneo hilo
walisema hawakusikia vurugu zozote usiku kwa hiyo huenda wauaji
walimchinja mbali na kwenda kuutupa mwili wake eneo hilo.
Mwili wa Pepetua ukitolewa shimoni na polisi.
Juni
9, mwaka huu, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura kuhusu kifo cha msichana
huyo ambapo alikiri kutokea.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
Mwili wa Pepetua baada ya kutolewa shimoni.
“Jeshi la
polisi tulipokea habari za kuwepo kwa mwili huo jana (Jumamosi) saa
sita na nusu, tukaenda na kuukuta ukiwa kwenye shimo la taka umechinjwa
shingoni na kiganja cha kushoto kilikatwa na kitu chenye ncha kali na
kwenye paji la uso alipasuliwa.
...Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari.
“Tuliuchukua
na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Mwananyamala. Vijana wawili wanaoishi
kwa Jaji Kileo ndiyo waliofika hospitali na kumtambua marehemu. Jaji
mwenyewe alikuwa safarini nje ya nchi, amerejea leo (juzi
Jumapili).“Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na
kifo hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande
Wambura.
kwa hisani ya GLOBAL PUBLISHER
0 comments:
Post a Comment