WADAU wa muziki nchini Kenya wameguswa na kifo cha msanii wa muziki wa kizazi
kipya nchini Tanzanian Langa Kileo, kilichotokea jana jioni katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Langa ambaye
alikimbizwa katika Hostali hiyo siku tatu zilizopita aliwahi kutamba na kibao
chake cha kwanza katika tasnia ya muziki iliyojulikana kwa jina la 'Langa matawi
ya juu', kifo chake kimekuwa gumzo katika mitaa mbalimbali ya jiji la
Nairobi.
Mwandishi Wetu akiripoti kutoka jijini Nairobi nchini
Kenya anasema kwamba wadau wa muziki wamepokea kifo cha msanii huyo kwa hisia
tofauti.
Jane Kimboi anasema kwamba alimfahamu Langa miaka mingi
iliyopita wakati akiwa katika kundi la (Wakilisha) iliyokuwa ikiongozwa na
Sarah Kaisi,ambapo baadaye waliweza kunyakuwa tuzo ya Coca Cola Popstars mwaka
2004.
"Hata hivyokundi la Wakilsha ilisambaratika mwaka mmoja
baadaye, kama ilivyo kwa wasanii mbalimbali Duniani Langa alipoteza ndoto zake
za kuwa msanii mkubwa ndani na nje ya Tanzania baada kujiingiza katika matumizi
ya dawa za kulevya"anasema Kimboi.
Joseph Omolo anasema kwamba kifo cha Langa
kimemwachia kumbukumbu ambayo hawezi kuisahau, ingawa marehemu hakuweza kutimiza
ndoto zake kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
"Langa ni msanii
pekee Afrika Mashariki aliyefanikiwa kupiga hatua kubwa baada ya kufanya maamuzi
ya kuacha kutumia dawa za kulevya, Langa aliweza kufungua taasisi yake ya
kuelimisha vijana juu ya matumizi ya dawa za kulevya"alisema
Omolo.
Alisema kwamba Langa aliweza kufungua taasisi hiyo
iliyoitwa 'Second Chance for African Addicts', na hata akafanikiwa kuachia wimbo
wake uliofahamika kwa jina la 'Kifo' wimbo huo ulikuwa na maudhui ya kuelemisha
jamii kuhusu madhara ya dawa za kulevya.
Omolo ambaye pia amewai kuwa mwathirika wa dawa za
kulevya alifafanua kwamba, Hata hivyo Langa alikuwa na mipango ya kujenga kituo
cha kulea na kusaidia vijana walioathiriwa na dawa za kulevya, ambapo angeweka
watalaamu wa ushauri nasaha na saikalojia pamoja na vifaa vya mazoezi
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/06/wakenya-wamlilia-marehemu-langa.html#ixzz2WJlsN3aL
Sunday, June 16, 2013
WAKENYA WAMLILIA LANGA .... NI KWANINI WANAMLILIA ZAIDI BAADA YA KIFO CHAKE? .... RIPOTI KAMILI HII HAPA
6:43 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment