Wastara Juma akiwa na mumewe Sadick Juma Kiwoloko ‘Sajuki’ enzi za uhai wake.
SIKU
chache baada ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma kumaliza eda na
kurejea Bongo akitokea Uarubuni ameanza kuona maruweruwe ndani ya
chumba alichokuwa akilala na mumewe marehemu, Sadick Juma Kiwoloko
‘Sajuki’, Risasi Mchanganyiko lina habari za uhakika.
Kwa mujibu wa Wastara siku hiyo akiwa amelala chumbani humo, usiku wa manane alihisi uwepo wa Sajuki kitandani kwake.
“Niliongea naye kwa kweli
siwezi kukumbuka haswa ni nini tulichoongea lakini tulikuwa katika hali
ya furaha sana,” alisema Wastara.
Pia, Wastara alisema kuwa
wakiwa katika maongezi yao, aliuchukua mkono wake na kuuweka juu ya
mwili wa Sajuki katika hali ya mapenzi na akapitiwa na usingizi.
“Asubuhi nilipoamka nilihisi
kama nilikuwa na Sajuki pale kitandani, kuangalia vizuri, mkono wangu
ulikuwa juu ya shuka badala ya mwili wa Sajuki,” aliongeza.
Hata hivyo, Wastara alisema
kuwa alihisi ni ndoto lakini alipochunguza alihisi kama kulikuwa na mtu
aliyekuwa amelala naye pale kitandani.
“Sijui kama ni maruweruwe,
ndoto au Sajuki alikuja kweli kitandani kwangu, kikubwa ninachokiamini
ni kwamba mapenzi kwa marehemu mume wangu ndiyo yamepelekea hali hiyo,”
alisema.
gpl
0 comments:
Post a Comment