Blogger Widgets

Saturday, October 6, 2012

ANGALIA PICHA ZA YA 25 MTU MZIMA RICK ROSS AKIKAMUA ON THE STAGE HAPA BONGO KWENYE SHOO YA SERENGETI FIESTA 2012 KATIKA VIWANJA VYA LEADERS USIKU WA KUAMKIA LEO.

Mtu mzima Rick Ross “The Boss” kutoka nchini Marekani akiwa jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar salaam ,akikamua ile mbaya na mashabiki wamepagawa vyakutosha kwa kila anachowaelekeza kufuata wanafuata jamaa amefunika mbaya, hiii ni mara yake ya kwanza kufanya onesho nchini Tanzania
Rick Ross hapa akiwaelekeza jambo mashabiki hawapo pichani wakati alipokuwa akiimba jukwaani usiku usiku wa kuamkia leo.
Rick Ross akiendelea kupagawisha mashabiki wake usiku huu kwenye viwanja vya Leaders
Watu wa usalama wakijaribu kudhibiti rapsha zilizokuwa zikijitokeza  kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kumuona mwanamuziki Rick Ross
Bibi Cheka na Stiko kutoka pande za TMK nao wakafanya mambo makubwa,
Wadau kutoka Serengeti wakifyurahia jambo katika burudani ya muziki.
Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko SBL Ephraim Mafuru na kutoka kushoto Meneja wa Masoko SBL Emmilian Rwejuna na Mdau Rawlence Mafuru pamoja na wadau wengine wakipozi kwa picha.
Wadau mbalimbali wakifuatilia burudani ya mwanamuziki Rick Ross wakati alipokuwa akitumbuiza,
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw Ephraim Mafuru akitangaza mshindi wa bahati nasibu ya magari mawili kwa mkoa wa Dar es salaam iliyoendeshwa katika matamasha yote ya Serengeti Fiesta mwaka huu kutoka kulia ni Bw. Mrisho kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha , Rugambo Rodney Meneja masoko wa Push Mobile na kushoto ni Mkurugenzi wa Clouds Entarteinment Bw Joseph Kusaga wakishuhudia tukio hilo
Pichani chini na juu mashabiki wakishangilia kwa nguvu wakati wanamuziki huyo akiimba jukwaani
Rachel Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na mmoja wa wacheza shoo wake  katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku  kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo pamoja na wasanii mbalimbali wakali wa nyumbani, mwanamuziki maarufu wa Hiphop kutoka nchini Marekani Rick Ross “The Boss” atahitimisha tamasha hilo kwa shoo kali usiku wa kuamkia leo .
 


 
 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani  usiku wa kuamkia leo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.

 Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.
 Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
 Baadhi ya Askari wakijaribu kuweka usalama wa kutosha kwa Mwanamuziki Rick Ross imara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lidaz Club,kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 201.
 Viwanja vya Lidaz palikuwa hapatoshi hata kidogo.
 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani vilivyo na madansa wake usiku wa kuamkia leo mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika kuhitimisha kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

0 comments:

Post a Comment