Blogger Widgets

Saturday, October 6, 2012

UNAJUA KWAMBA BONDIA ORLANDO CRUZ NI SHOGA

Orlando Cruz kulia akizichapa na  Cornelius Lock kuwania ubingwa wa  NABO Latino uzani wa Featherweight.

SAN JUAN, Puerto Rico
BONDIA wa uzani wa ‘featherweight’ raia wa Puerto Rico, Orlando Cruz amekuwa nyota wa kwanza wa masumbwi kuanika hadharani ukweli kwamba yeye ni shoga.
Cruz, 31, alikuwa sehemu mabondia wa nchi hiyo walioshiriki katika michezo ya Olimpiki 2000 na kupambana mapambano kadhaa ya kuwania ubingwa dunia wa WBO.
"Nimekuwa mpambanaji ulingoni kwa zaidi ya miaka 24 sasa nab ado ningali nataka kuendelea katika hilo, lakini ni bora nikawa wazi kuhusu masuala yangu binafsi," alisema Cruz, ambaye ameshinda mapambano 18 kati ya mara 22 alizopanda ulingoni.
"Mimi daima najisikia na nitaendelea kujisikia fahari kuwa raia wa Puerto Rico. Na daima mimi nimekuwa na nitaendelea kujivunia kuwa mwanaume shoga."
Kukiri ushoga kwa Cruz, kumekuja wiki mbili tu kabla ya mkali huyo kupanda ulingoni kumvaa Jorge Pazos kuwania ubingwa wa WBO Latino uzani wa ‘featherweight’ huko Florida, pambano linaloweza kumpa tiketi ya kuwania ubingwa wa dunia.
Cruz aliongeza katika mahojiano yake kuwa: "Nataka kujaribu kuwa mtu wa kuigwa na vizazi vyote wakiwamo watoto katika suala zima la mchezo wa masumbwi ya kulipwa na si vinginevyo."
Bingwa mara mbili wa zamani wa dunia Emile Griffith, aliwahi kukiri kuwa yeye ni shoga katika mahojiano aliyoyafanya na jarida la Sports Illustrated, lakini alifanya hivyo wakati akiwa ameshastaafu mchezo huo.

0 comments:

Post a Comment