Blogger Widgets

Wednesday, October 24, 2012

HILI NDIO GARI JINGINE AMBALO KUNDI LA KINA LORD EYES LINATUHUMIWA KUIBA.

.
Siku moja baada ya Polisi kutangaza kwamba inamshikilia msanii Lord Eyes na mwenzake mmoja kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz huku wakikabiliwa na mashtaka mengine zaidi ya 30, walioibiwa wanaanza kujitokeza.

Wa kwanza ni mama mmoja aitwae Jackline Fred Zacharia ambae anadai aliibiwa baada ya gari lake kufunguliwa Mbezi Makonde Dar es salaam october 5 2012 yeye alipokua ameingia kanisani.
Baada ya kukuta kaibiwa vitu mbalimbali ikiwemo pochi, vipodozi, begi la mtoto la shule na hati ya kusafiria alikwenda Polisi Kawe.

Muda mfupi kabla ya kwenda kituo cha Polisi Jackline anadai kulikua na gari jingine pembeni yao aina ya Opa la dada mmoja ambalo walilivunja pia na kumuibia simu mbili ambapo baada ya kuiba wezi hao waliingiza line zao kwenye hizo simu kitu ambacho kilisaidia yule dada alieibiwa kuona namba za wezi na kuanza kuwafatilia na kuwapigia simu, msichana Kurushinde ambae ni mtuhumiwa alipokea simu na baadae kukubali kwamba wao ndio wamehusika na huo wizi
Jackline kasema baada ya Kurushinde kukiri hivyo kwa dada wa Opa na yeye alipewa namba ya simu ya Kuldish ambae alikiri kweli anavyo vitu vingine vilivyoibiwa kwenye gari la Jackline pia.

Jackline alianza kufatilia kupata passport yake tu baada ya kuamua kuachana na vile vitu vingine vilivyoibwa, walipompigia Kurushinde akasema anataka alipwe laki moja ili arudishe passport hivyo Jackline ilibidi amtumie hiyo pesa kupitia huduma za simu zinazotolewa na moja kati ya makampuni ya simu za mkononi ambapo baada ya kutuma hiyo pesa ndio wakaona jina lake vizuri ambapo baada ya kutumiwa Kurushinde alitaka aongezewe pesa.
 
Pamoja na kutuma hiyo laki moja ya kwanza, Jackline hakupata passport yake, baada ya muda kupita juzi ndio wakawa wamesikia Kamanda wa polisi akiongea kwenye AMPLIFAYA kuhusu tuhuma za kundi la kina Lord Eyez hivyo wakaja Clouds Fm na kuelekezwa kwamba watuhumiwa wako kituo cha Polisi Osterbay, walipokwenda kweli wakamkuta Kurushinde ambae alikiri kwamba anavyo vitu vyao vyote lakini maaskari wakawaambia kina Jack wasubiri kwanza mpaka kina Kurushinde wahojiwe vizuri.

CHANZO NA MILLARD AYO-OFFICIAL WEBSITE

0 comments:

Post a Comment