Blogger Widgets

Wednesday, October 3, 2012

MTOTO ANAYEKADIRIWA KUWA NA MWEZI MMOJA AKUTWA AMETUPWA

 Msamaria mwema aliyrfahamika kwa jina moja Lina akiwa amembeba mtoto ambaye alikutwa ametupwa katika bomba la Nyumba moja wilayani Sengerema.
                                     Mtoto ambaye alitupwa akionekana katika picha..
 Umati wa watu waliofika kwenye tukio la utupwaji wa mtoto mchanga wakishangaa sana kutokana unyama huo ambao haukubaliki kwa jamii ya Kitanzania.
                              Sura ya Mtoto aliyetupwa kama inavyoonekana pichani.

MTOTO mchanga anayekadiliwa kuwa na umri wa mwezi mmoja amekutwa ametupwa kwenye boma la nyumba moja iliyopo katika kata ya Ibisabageni wilayani sengerema mkoani mwanza.

Tukio hilo limetokea jumatatu majira ya asubuhi katika kata hiyo ambapo mtoto huyo amekutwa ametupwa na msamalia mwema ambaye ni mtoto aliyefahamika kwa jina la KUBUNGA na kuamua kutoa taarifa kwa ndugu jamaa na ndipo walipofika eneo la tukio.

Akielezea kuhusu tukio hilo amesema kuwa wakati anapita eneo hilo alisikia sauti ya mtoto ikilia  na ndipo aliposogea karibu na kukuta mtoto huyo mchanga akiwa amelazwa chini.

Naye Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bw. JAPHET MASHALA  ambaye alikuwepo eneo la tukio amelaani kitendo hicho na kusema ni cha kinyama na kuwaomba wananchi kuwa na moyo wa ubinadamu wa kuthamini maisha ya wengine kwani mtoto huyo hana hatia yoyote.

Hata hivyo mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio juhudi za kumtafuta aliyetenda unyama huo zilikuwa zinaendelea ili kumfikisha katika vyombo vya dola. Chanzo: B Plus Blog

0 comments:

Post a Comment