Blogger Widgets

Monday, August 27, 2012

JINSI MASHEHE WALIVYOKWEPA KUHESABIWA KWENYE SENSA.

Posted: 28th August 2012 by yusha

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno wa pili kutoka kulia.
Zoezi la sensa ya watu na makazi kwenye mkoa wa Kigoma lilipata ugumu kutokana na waumini wa dini ya kiislamu wanaopinga kuhesabiwa kukimbilia misikitini hivyo kutofikiwa na makarani waandikishaji.
Mkuu wa wilaya Kigoma Ramadhani Maneno amesema kwenye pitapita yao kufanya tathmini wamekutana na ugumu huo na tayari wameanza kuufanyia kazi, maeneo ambayo wamegundua tatizo hilo ni pamoja na Mwandiga na Katonga ambapo licha ya kutaka kuongea na viongozi wa misikiti hiyo, wameshindwa kupata ushirikiano wowote hivyo  amesema kamati ya ulinzi na usalama inatarajia kukaa kujadili ili kuona hatua za kuchukua.

hii ni moja ya baadhi ya picha zilizosambaa za waumini wa dini ya kiislamu kupinga ishu ya sensa.
Amekaririwa akisema “kuna baadhi ya viongozi wa kiislam wameshawishi waislam wenzao kwenda kulala misikitini ili kusiwe na nafasi tena kwa makarani wa sensa kuingia misikitini, nilipojaribu kwenda kwenye msikiti wa Mwandiga kujaribu kushawishi niongee na viongozi wao, sikufanikiwa”
Mwandishi Fadhili Abdallah anasema Mkuu huyo wa wilaya amethibitisha jumla ya kaya 40 kati ya 64 kwenye kijiji cha Bubango kata ya Bitale Kigoma Vijijini, zimekataa kuandikishwa kufuatia maelekezo ya viongozi wa kaya hizo.

0 comments:

Post a Comment