Blogger Widgets

Friday, August 10, 2012

POINT ALIYOITOA NIKKI WA PILI KUHUSU KUANDIKA JINA BADALA YA NAMBA KWENYE GARI KAMA HIVI.

Posted: 10th August 2012 by yusha shabani
Pipi na Nikki wa II kwenye making the video ya kiujamaa.

Najua kwa Tanzania sasa hivi hii ni ishu mpya ambayo imetangazwa na serikali kwamba wenye uwezo wa kulipa milioni 5 kwa miaka mitatu wanaweza kuandika majina yao kwenye magari wanayomiliki badala ya namba.
Kupitia millardayo.com mastaa kadhaa wamesikika wakiiongelea hii ishu ambapo asilimia 90 wamekataa kwamba hawawezi kuweka.
Mtu mpya kuongea nae kuhusu hili ni rapper Nikki wa II ambae namkariri akisema “kwa mimi naona haina umuhimu lakini pia kama ni mtu maarufu na una hela nyingi unasupport uchumi wa nchi yako kwa hiyo hiyo milioni tano yako unaweza kuitoa na kwa kulipia kwako kuna watu watapata huduma za Afya, maji na mengine kwa sababu ya hiyo kodi”
Hili ni moja kati ya magari ya watanzania yaliyoandikwa majina badala ya namba, ni la Davis Mosha aliekua kiongozi wa Yanga. hii ni picha ambayo ilisambaa kwenye website na blogs mbalimbali Tanzania wakati wa uchaguzi wa Yanga.


“Kwa mtu maarufu unaweza ukaitumia kama njia ya kurudisha kwenye jamii kile ambacho unakipata, kama nitafanikiwa hela nyingi nitatoa kama kodi ya kuchangia nchi yangu ili mambo kama Afya, elimu na mengine yaweze kuboreka na pato la nchi likue, nitaiunga mkono hii ishu kwa angle hiyo na nitatoa hiyo pesa kama serikali haitakua na rushwa kwa sababu nisije nikatoa kwa ajili ya watanzania wenzangu lakini pesa zikaishia kwenye mikono ya wasiostahili”

0 comments:

Post a Comment