Blogger Widgets

Thursday, January 31, 2013

#BREAKING: TAARIFA KUHUSU JAHAZI LILILOZAMA NUNGWI LEO JANUARY 31 2013 LIKIWA NA WATU 32 IKO HAPA

Ajali ya Nungwi september 2012.

Taarifa zilizo kwenye headlines wakati huu ni kuhusu kuzama kwa Jahazi liitwalo Sunrise likitokea  Tanga kulekea visiwani Zanzibar likiwa na abiria 32 ambapo limezama kwenye lile eneo la Nungwi ambalo ni hatari siku zote.
Namkariri Kamanda wa Polisi Zanzibar akisema “tayari tumeshapokea watu 21 waliookolewa wakiwa wazima na hakuna maiti iliyopatikana mpaka sasa hivi, waliokuwemo kwenye chombo ni watu 32 hivyo watu bado watu 11 hawajulikani walipo”
Endelea  kupita hapa theHOODinfotainment  kwa taarifa zaidi zitakazotufikia wakati wowote

0 comments:

Post a Comment