Blogger Widgets

Friday, January 4, 2013

RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII- UDOM ATIWA MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 15.6

RAISI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM) IDD MOHAMED NA WAZIRI WAKE WA FEDHA IBRAHIM MATATA WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI 6,MALI YA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)


TAARIFA ZINASEMA KUWA RAISI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII, SANAA NA LUGHA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU ANAYESOMA BCOM ACCOUNTINGANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA IDD MOHAMED ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KITUO CHA POLISI UDOM KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI 6.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA JANA SIKU YA ALHAMISI AKIWA NA MWENZAKE AMBAYE PIA ALIKUWA WAZIRI WA FEDHA WA KITIVO HIKO IBRAHIM MATATA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU BCOM ACCOUNTING NA KUFIKISHWA KATIKA KITUO HIKO CHA POLISI.
MARA BAADA YA KUKAMATWA WALIKUTWA NA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 7 LAKI 2 NA 24 ELFU.(Shilingi 7,224,000 ZA Kitanzania.) Na fedha hizo zilitolewa kwenye account ya serikali ya wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha na kupelekwa katika Akaunti ya Mtu Binafsi ambaye ni Waziri wa Fedha wa Kitivo hiko Ndugu Ibrahim Matata.

Chanzo hicho kiliendelea Kujuza kuwa Awali Raisi Huyo Anahusika na kosa la kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni 1 na laki 1 katika Duka lililopo Katika Bweni namba 13 (Block 13 ).

Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa Fedha walikamatwa Jana na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM tayari kwa Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa ili kuweza Kufikishwa mahakamani

Habari zaidi ambazo Lukaza imezipata kutoka katika Vyanzo vya habari Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake Wa fedha watafikishwa Mahakamani Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa Shilingi Milioni 15 na laki 6 ambapo waliweza kuzitoa na kuweka katika akaunti ya Waziri Wa Fedha Ibrahim Matata na kufanikiwa kuchukua Sh Milioni 7 laki 2 na Ishirini na Nne elfu ambazo ndio walikamatwa nazo Mkononi.

Hatimaye Bunge la Serikali ya Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii ,Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma linatarajiwa kukaa leo Saa 10 Jioni ili kuweza kutoa uamuzi wa Kumvua madaraka na kufikisha baadhi ya Ushaidi wa Sauti wakati Raisi huyo akiomba Rushwa katika Duka lililopo Block 13.

0 comments:

Post a Comment