Blogger Widgets

Friday, January 11, 2013

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2012 HAYA HAPA

Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo ametangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, ambapo kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012.
Matokeo hayo yametangazwa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851, ikiwa ni upungufu wa watahiniwa 36,240 ikilinganishwa na mwaka 2011 ambao walikuwa 466,567.
“Watahiniwa 386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244 na wavulana 199,027, watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825” amesema Mulugo.

0 comments:

Post a Comment