Blogger Widgets

Thursday, January 3, 2013

PICHA 4 ZA USHAHIDI WA BALOTELLI KUTAKA KUPIGANA NA KOCHA MANCINI MAZOEZINI LEO JAN 3.


Leo asubuhi Kocha wa Manchester City Roberto Mancini na mchezaji wake Mario Balotelli walitaka kupigana baada ya kocha Mancini kukasirishwa na kitendo cha Balotelli kumchezea rafu mchezaji mwenzake Scott Sinclair wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na mechi ya Watford.
Baadhi ya makocha waliokua karibu ndio waliamua huo ugomvi ambao pamoja na kwamba Balotelli ndio alikua na makosa alikua mbishi wa kutokukubali au kukiri kosa na badala yake ndio akaendelea kupandishiana na Mancini tena mbele ya wachezaji wenzake.
Baada ya hapo Mario aliondoka zake na kuingia kwenye gari lake aina ya Bentley na kukutana na mashabiki nje ya uwanja waliokua wanahitaji awachoree autographs kisha akaondoka.
Wengi wamekua wakimshauri Mancini amuuze Balotelli lakini amekua akikataa na hata kwenye interview na Gazzetta mwezi uliopita Mancini alikaririwa akisema “nafikiri Balotelli ataendelea kukaa Man City ila inabidi akue  aache utoto, uhusiano wangu mimi na yeye ni mzuri siku zote hata akinikosea ila kwa sasa rungu la kazi halitakua na huruma tena kwake”
.
.
.

0 comments:

Post a Comment