Blogger Widgets

Wednesday, January 30, 2013

MUIGIZAJI MATUMAINI ANA HALI MBAYA NCHINI MSUMBIJI ANAHITAJI MSAADA WA HARAKA

Mchekeshaji na muigizaji maarufu Tanzania Tumaini Martin maarufu kwa jina la Matumaini anaumwa na ana hali mbaya sana chini Msumbiji na inasemekana amevimba miguu na tumbo na mwili mzima kukosa nguvu, hivyo msanii huyo anahitaji msaada wa haraka ili apate nauli ya kurudia nchini na kuja kupata matibabu.Taarifa rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha waigizaji taifa Mike Sangu zinasema "msanii mwenzetu matumaini bado anaumwa sana na bado yupo Msumbiji mpaka sasa na kitu ambacho kinamsumbua ni kuvimba miguu na tumbo na akiwa hana uwezo wa kujitibia wala nauli ya kurudia nchini". Taarifa za awali zinasema msanii huyo aliingia Msumbiji kwa ziara ya kisanii na akiwa huko alimpata jamaa wa huko na kuamua kufanya maisha yake nchini humo. Wenzake waliokwenda nae nchini humo walirudi nchini lakini yeye aliamua kubaki ili kuanza maisha mapya.Kwa wale watakaoguswa na tatizo lake wanaweza kumsaidia kupitia Tigo pesa kupitia mwenyekiti wa waigizaji taifa ndugu Michael Sangu kwa namba hizi +255718951355.
mungu amsaidie apone haraka na kurudi katika majukumu yake ya kila siku.

0 comments:

Post a Comment