Baba Mtakatifu, Papa Benedict XVI KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, |
Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa
ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne
ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.
Katika
taarifa yake, Papa amesema amefikia uamuzi huo ambapo sasa ana umri
wa miaka 85.Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo
wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe
28 Februari, mwaka huu saa mbili kamili asubuhi.
Wachambuzi
mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano
mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka
Afrika. Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama
mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki,
linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima.
Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye
alichukua nafasi ya Benedict XVIkama Kardinali-Askofu wa
Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.
0 comments:
Post a Comment