Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Monday, September 30, 2013

UKWELI JUU YA MAISHA HALISI YA DIAMOND WAANIKWA ... NI HUU HAPA

UKWELI JUU YA MAISHA HALISI YA DIAMOND WAANIKWA ... NI HUU HAPA

Written By Emmanuel Shilatu on Saturday, September 28, 2013 | 9:25 PM



Mdogo wa Diamond ameamua kumuumbua kaka yake.Kayaanika maisha yake yote tangu akiwa underground hadi star...

Dodo anadai Diamond alikuwa ni muuza supu ya ngozi, mswaki alikuwa anapiga mara moja kwa wiki...

Inadaiwa Diamond alikuwa ni mnywa Gongo, chokoraa na mengine kibao ambayo mdogo wake kaamua kuyaanika....
- See more at: http://shiladeux.blogspot.com/2013/09/ukweli-juu-ya-maisha-halisi-ya-diamond.html#sthash.HkXe4LOV.dpuf
Mdogo wa Diamond ameamua kumuumbua kaka yake.Kayaanika maisha yake yote tangu akiwa underground hadi star...

Dodo anadai Diamond alikuwa ni muuza supu ya ngozi, mswaki alikuwa anapiga mara moja kwa wiki...

Inadaiwa Diamond alikuwa ni mnywa Gongo, chokoraa na mengine kibao ambayo mdogo wake kaamua kuyaanika.... - See more at: http://shiladeux.blogspot.com/2013/09/ukweli-juu-ya-maisha-halisi-ya-diamond.html#sthash.HkXe4LOV.dpuf
Mdogo wa Diamond ameamua kumuumbua kaka yake.Kayaanika maisha yake yote tangu akiwa underground hadi star...  Dodo anadai Diamond alikuwa ni muuza supu ya ngozi, mswaki alikuwa anapiga mara moja kwa wiki...  Inadaiwa Diamond alikuwa ni mnywa Gongo, chokoraa na mengine kibao ambayo mdogo wake kaamua kuyaanika.... 

ANGALIA PICHA YA MWANAUME ANAYEWEZA KUKAANGA KUKU KWENYE MAFUTA KWA MIKONO YAKE BILA KUUNGUA



m1

Mwanaume huyo (52) mkazi wa jiji la Chiang Mai ambaye ni mpishi huko Thailand, ana uwezo wa ajabu wa kuzamisha mikono yake katika mafuta yenye moto wa digrii 480 bila kuungua na amedai kuwa huwa hasikii maumivu ya aina yoyote wala ngozi ya mikono yake haidhuriki na mafuta ya moto mkali.
Mr Trichan anashikilia rekodi ya dunia kwa kukaanga vipande 20 vya kuku katika mafuta ya moto wa 480c ndani ya dakika 1.

m2
Kutokana na maajabu hayo ya mikono yake mwanaume huyo amepata umaarufu wa kimatifa uliompa faida zaidi katika biashara yake kwani watu mbalimbali kutoka pande tofauti za dunia wamekuwa wakitembelea ofisi yake ya chakula “Fried Chicken Iron Hands Man” ili kushuhudia jinsi Kann anavyoweza kutumia mikono yake kuchota kuku kutoka kwenye mafuta ya moto. 
m3
m4
Mwanaume huyo na mke wake wamekuwa wakisafiri duniani kuonesha maajabu hayo ambayo hajui ni jinsi gani ameweza kufanya anachokifanya na mikono yake, lakini anafuraha sababu inamuongezea wateja zaidi katika biashara yake kila siku.
Mr Trichan aligundua kipaji chake hicho cha kipekee miaka nane iliyopita baada ya kumwagikiwa na mafuta ya moto kwa bahati mbaya lakini hakudhurika.
Onyo: Usijaribu hii nyumbani.NA KILELE CHA HABARI
Mtazame hapahapa

JimmyMaster ft Kisuke Matoke & SpacDawg-Bado Nahaso

Download "Bado Nahaso" wimbo wa JimmyMaster akiwa amemshirikisha Kisuke Matoke & SpacDawg mzigo toka studio za Noizmekah Arusha bofya HAPAHAPA kuisikiliza ngoma na kwa mawasiliano zaidi check na Jimmy Master aka Mnyampaa kwa nambari +255 655 499 318

WEMA AENDA KUFANYIA BETHIDEI CHINA!

Wema Isaac Sepetu (kulia) akipozi na Aunty Ezekiel wakati wa pati ya ‘bethidei’ yake.
Na Imelda Mtema

JEURI ya Fedha! Wema Isaac Sepetu a.k.a Madam ameenda Hong Kong nchini China na kufanyia huko bonge la pati ya ‘bethidei’ yake wakati akitimiza umri wa miaka 25 huku staa mwenzake, Aunty Ezekiel akiungana naye akitokea Dubai.…

Wema Isaac Sepetu (kulia) akipozi na Aunty Ezekiel wakati wa pati ya ‘bethidei’ yake.
Na Imelda Mtema
JEURI ya Fedha! Wema Isaac Sepetu a.k.a Madam ameenda Hong Kong nchini China na kufanyia huko bonge la pati ya ‘bethidei’ yake wakati akitimiza umri wa miaka 25 huku staa mwenzake, Aunty Ezekiel akiungana naye akitokea Dubai.

...Madam ndani ya Hong Kong.
Habari kutoka Hong Kong zilisema kuwa Madam alifanya tukio hilo Ijumaa iliyopita Septemba 27, mwaka huu ambapo aliongozana na ndugu yake aliyetajwa kwa jina moja la Bite huku Aunt akiungana naye akitokea kwa mumewe, Sunday Demont huko Dubai.
Ijumaa Wikienda lilipenyezewa picha za tukio zikiwaonesha Wema, Aunt na ‘kampani’ zao wakipiga vinywaji vikali na bata nyingine za kufa mtu.

...Madam 'akishow' love.
Tukio hilo lilisababisha Wema kupokea hongera nyingi kutoka kwa mastaa wenzake, mashabiki na watu wa kawaida akisifiwa kuwa amewaziba midomo wasanii wenzake kwa kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Hong Kong.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kutoka Hong Kong, Aunt alisema kuwa alikwenda Dubai kwa mumewe lakini alikuwa na taarifa kuhusu pati ya Wema hivyo alivyofika Dubai alianza taratibu za safari za kuelekea Hong Kong.

Thursday, September 26, 2013

ANGALIA PICHA ZA AWALI ZA KWANZA ZINAZO ONESHA JINSI WESTGATE ILIVYO HARIBIWA.


Carnage: The collapse came on Monday, shortly after large explosions rang out followed by billows of smoke

Carnage: The collapse came on Monday, shortly after large explosions rang out followed by billows of smoke
Destruction: Cars are strewn among the carnage, which was caused by Kenyan soldiers who fired rocket-propelled grenades inside the complex, knocking out a support column, a government official said
Destruction: Cars are strewn among the carnage, which was caused by Kenyan soldiers who fired rocket-propelled grenades inside the complex, knocking out a support column, a government official said
Conflicting reports: A minister said the terrorists had set mattresses on fire, causing the roof to collapse
Conflicting reports: A minister said the terrorists had set mattresses on fire, causing the roof to collapse
One soldier told the Daily Mirror: 'I have seen many bad things, but this will haunt me
Still smouldering: Smoke rises over the mall on Thursday morning as a forensic examination begins inside
Still smouldering: Smoke rises over the mall on Thursday morning as a forensic examination begins inside
Assessing the damage: Kenyan government officials accompanied by armed security officers tour an outside upper level near a collapsed floor of the Westgate mall
Assessing the damage: Kenyan government officials accompanied by armed security officers tour an outside upper level near a collapsed floor of the Westgate mall

Surveying the scene: A Maasai man looks out over the smouldering mall from an overlooking building
Surveying the scene: A Maasai man looks out over the smouldering mall from an overlooking building

Daily Mail
 

CHEKI WACHINA HAWA WAKITAKA SIFA KUINGIZWA KATIKA RECORD YA DUNIA WALIVYOUMBUKA!

Watu wengine kwa kutaka sifa! Hii ni moja ya Record zilizo recodiwa si kwasababu ya kufanikiwa hapana ni baada ya kushidwa kuweka Record ya MNARA MKUBWA ULIOTENGENEZWA NA WATU kutoka nchini china na kuambulia aibu tosha....

UFUSKA WA KUTISHA!

 
Stori: Brighton Masalu

HAKIKA wazazi wanaosomesha mabinti lazima wataumia wakisoma kisa hiki kilichojaa ufuska wa kutisha, Amani linakupa kwa undani.

Mwanafunzi wa kike aliyetajwa kwa jina moja la Agness, hivi karibuni alijifungia chumbani na njemba mmoja aitwaye Colvin na kufanya ngono zembe huku wakijirekodi na kujipiga picha za video wakidai ni kumbumbu yao. Kisa hicho kinachoumiza kwa wazazi wanaolipa karo ili watoto wao wasome,…
Stori: Brighton Masalu
HAKIKA wazazi wanaosomesha mabinti lazima wataumia wakisoma kisa hiki kilichojaa ufuska wa kutisha, Amani linakupa kwa undani.
Mwanafunzi wa kike aliyetajwa kwa jina moja la Agness, hivi karibuni alijifungia chumbani na njemba mmoja aitwaye Colvin na kufanya ngono zembe huku wakijirekodi na kujipiga picha za video wakidai ni kumbumbu yao.Kisa hicho kinachoumiza kwa wazazi wanaolipa karo ili watoto wao wasome, kimetokea Kiwalani jijini Dar baada ya mwanafunzi huyo anayedaiwa kusoma chuo kimoja jijini humo kukacha masomo.
Inadaiwa kuwa binti huyo aliaga kwa wazazi wake kwamba anakwenda chuoni lakini hakufika na kukutana na mpenzi wake huyo na kujifungia chumbani.Wakiwa chumbani kwa siku nzima wakifanya vitendo vingi vichafu ambavyo si rahisi kuviandika gazetini, hatimaye picha za video walizokuwa wakijirekodi zilivuja na kutua katika ofisi za gazeti hili.
Mwandishi wetu alianza kufanya utafiti na hatimaye kupata habari za Colvin ambaye inadaiwa kuwa ni mchezo wake kuwarekodi wanawake anaokuwa nao faragha. “Huyu jamaa amezidi, tumemuonya mara kadhaa lakini amekuwa mgumu, anawadhalilisha wanafunzi na wake za watu wakati mwingine bila ya wao kujua kama anawarekodi,” alisema mmoja wa watu wanaomfahamu kijana huyo.
Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu aliwatafuta wahusika wanaoonekana katika video hiyo ili kutaka kujua sababu ya kufanya hivyo.Colvin ambaye ndiye mtuhumiwa namba moja wa uchafu huo, alikuwa wa kwanza kuulizwa. Hata hivyo, alijibu kwa jeuri kwa madai kuwa haoni ubaya wa kufanya jambo hilo kwani Agness ni mpenzi wake wa muda mrefu. “Ni kweli nilifanya hivyo, Agness ni mpenzi wangu, nimezaa naye, hivyo sioni ubaya kufanya mapenzi na mzazi mwenzangu huku tukijirekodi kama kumbukumbu yetu,” alisema Colvin na kukata simu huku akimtaka mwandishi wetu kutomfuatilia.
Kwa upande wake, Agness awali alijaribu kutaka kumhonga mwandishi wetu fedha ili asichapishe picha hizo gazetini.
“Basi nikutumie hela usitoe hiyo habari na je, tukutane wapi ili nikupe hiyo hela…?” ilisomeka meseji ya Agness.
Msichana huyo alipoona kuna ugumu wa suala hilo kutimia akabadili maneno na kusema:
 “Kwani kuna ubaya gani kujirekodi tukifanya mapenzi na mwandani wangu? Kama amekuwa akifanya hivyo kwa wanawake wengine miye sijali,” alisema Agness.
Kama vile haitoshi, Agness akaanza kutukana matusi mazito kwa mwandishi wetu ambayo hayaandikiki gazetini.

Magaidi wafanya shambulio lingine tena nchini Kenya

Watu wanaodhaniwa kuwa magaidi wamevamia kituo cha Polisi katika Mji wa Mandera nchini Kenya kwenye mpaka na Somalia na kuwaua polisi wawili, watatu wamejeruhiwa vibaya na baadaye kuchoma magari zaidi ya 11.
Jana pia kulikua na shambulio sehemu inaitwa Wajir kwenye soko ambapo mtu mmoja alifariki… kuna taarifa nyingine zinazidi kuja ila nasubiria tu uthibitisho ili niwezi kuziweka hapa mtu wangu.

chanzo:  millardayo.com

Monday, September 23, 2013

DAR HOFU YATANDA

 
 
Wananchi walionusurika katika shambuli hilo.

 

 

 

Moshi mkubwa ukifuka kutoka katika jengo la Westgate, jijini Nairobi jana.
Stori: Mwandishi Wetu
Mauaji ya kihistoria yaliyotikisa Jiji la Nairobi, Kenya, yamechagiza mshtuko wa aina yake nchini Tanzania na sasa hofu imetanda ndani ya Dar es Salaam hususan kwenye majengo ambayo huchukua watu wengi kila siku.

Mauaji ya kihistoria yaliyotikisa Jiji la Nairobi, Kenya, yamechagiza mshtuko wa aina yake nchini Tanzania na sasa hofu imetanda ndani ya Dar es Salaam hususan kwenye majengo ambayo huchukua watu wengi kila siku.

Kitendo cha Kikundi cha Al-Shabab kukiri kuhusika na utekaji wa Jengo la Westgate, Nairobi, Jumamosi iliyopita na kufanya mauaji ya kutisha, ukijumlisha na sababu walizotoa za uharamia huo, kwa pamoja inafanya Dar isiwe salama.

Al-Shabab, imetoa sababu ya kuivamia Kenya kwamba nchi hiyo imekuwa ikiingilia mipango yao ya ugaidi nchini Somalia.

Taarifa ya kikundi hicho chenye makao yake Somalia, imeeleza: “Kenya waondoe majeshi yao Somalia, wasipofanya hivyo, tutaendelea kufanya utekaji zaidi.”
SABABU YA DAR KUVAMIWA

Mosi; Mwaka jana,…
Kitendo cha Kikundi cha Al-Shabab kukiri kuhusika na utekaji wa Jengo la Westgate, Nairobi, Jumamosi iliyopita na kufanya mauaji ya kutisha, ukijumlisha na sababu walizotoa za uharamia huo, kwa pamoja inafanya Dar isiwe salama.
Al-Shabab, imetoa sababu ya kuivamia Kenya kwamba nchi hiyo imekuwa ikiingilia mipango yao ya ugaidi nchini Somalia.
Taarifa ya kikundi hicho chenye makao yake Somalia, imeeleza: “Kenya waondoe majeshi yao Somalia, wasipofanya hivyo, tutaendelea kufanya utekaji zaidi.”
SABABU YA DAR KUVAMIWA
Mosi; Mwaka jana, Kikundi cha Al-Shabab kiliitishia Tanzania kusitisha shughuli za burudani, vinginevyo kitateketeza kumbi zote za starehe nchini, hususan Dar.
Agizo hilo la Al-Shabab lilipuuzwa, hivyo kuiweka hai hofu kwamba kwa uthubutu waliouonesha Nairobi, wanaweza kuuendeleza Dar.
Pili; Tanzania inapita katika njia za Kenya katika ushiriki wa kurejesha amani kwenye mataifa yenye machafuko.
Tanzania inashiriki kurejesha amani Darfur, Sudan, DRC na kadhalika, hivyo imekuwa ikitazamwa kwa jicho baya na vikundi vya uasi katika nchi hizo.
Kikundi cha Janjaweed nchini Sudan, kinaweza kuthubutu kuingia nchini na kufanya utekaji, kutokana na hasira zake dhidi ya Tanzania kwa vile askari wa JWTZ, ndiyo kikwazo kwao kila wanapopanga uharamia wao.
Chuki ya waasi wa kikundi cha M23, DRC, dhidi ya Tanzania ipo wazi, kimekuwa kikielekeza vitisho vya dhahiri kwa serikali mpaka kuilazimisha itoe matamko kujibu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, mara kwa mara hutoa matamko kujibu maneno ya M23.
Bungeni wakati wa vikao vya bajeti mwaka huu, Membe alitumia muda mwingi kujibu waraka wa M23 ambao waliutuma nchini, wakieleza kuwa ni ujumbe kutoka kwa Mungu, wakiionya Tanzania kutopeleka majeshi DRC, vinginevyo itakiona cha moto.
Hata hivyo, baada ya majibu ya Membe, M23 walihamishia mashambulizi yao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, wakiitishia Tanzania.
Baadhi ya ‘twiti’ za M23, siku moja baada ya Membe kusisitiza bungeni kwamba Tanzania itaenda DRC, mojawapo ilisema: “Membe usiwadanganye watu, mnakuja DRC kuweka petroli kwenye moto, hamji kutafuta amani.”
Twiti nyingine inasomeka: “Hatutishwi na scout (askari chipukizi), Tanzania leteni majeshi yenu halafu mtaona.”
Hatari kubwa zaidi ni kwamba M23, walitishia kuingia nchini na kufanya mashambulizi, wakitamba wana uwezo mkubwa wa kufanya hivyo.
Kutokana na hatari hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ‘alitwiti’, akionya kwamba M23 walikuwa ‘wanatwiti’ wakiwa Dar es Salaam, hivyo ni dhahiri kuwa kundi hilo lilikuwa limeshaingia nchini.
Kauli hiyo ya Zitto, ilikuwa inaweka wazi namna taifa letu lilivyo hatarini, kwani maadui wanaweza kuingia nchini na kupanga mashambulizi dhidi yetu bila sisi wenyewe kujua.
MAENEO HATARI
Kwa tathmini ya kile kilichotokea Nairobi, ndani ya Jiji la Dar wananchi wamehofia maeneo yenye watu wengi kwamba yanaweza kutekwa na kusababisha maafa kuliko yale ya Jengo la Westgate.
Pius Matilido, 41, mfabiashara aliyejitambulisha kwamba ni mfuatiliaji mzuri wa habari za kimataifa, alisema kuwa vyombo vya usalama vya Tanzania, viyaangalie majengo ya Mlimani City, Quality Centre, Soko la Kariakoo, Golden Jubilee Tower, Benjamin Mkapa Tower na mengine ambayo huchukua watu wengi kwa siku.
“Hata Millennium Tower na Ubungo Plaza ni ya kuyaangalia sana, magaidi hawashindwi kuingia nchini na kufanya uharamia kama Kenya,” alisema Matilido.
Kwa upande wa Nancy Nehemia wa Mwananyamala, Dar es Salaam, alisema kuwa anaona Tanzania haipo salama, hasa anapoangalia matukio ya ujambazi wanavyoteka magari na kuwapora abiria.
“Kama majambazi tu wanafanya Watanzania wasisafiri kwa amani, inakuwaje M23, Al-Shabab au Janjaweed wakija? Tukio la Nairobi ni shule kwa vyombo vya usalama kudumisha ulinzi wa nchi,” alisema Nancy.
SERIKALI YAKAA MGUU SAWA
Serikali kupitia kauli ya msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Eric Komba ni kama imekaa mguu pande mguu sawa kutoka na tishio la ugaidi. 
“Tupo imara, tunadumisha ulinzi kama kawaida, tutawadhibiti magaidi,” alisema Komba.
NI MAUAJI YA KIHISTORIA KENYA
Tukio la Al-Shabab kuvamia Jengo la Westgate na kuua raia ni la aina yake katika historia ya Kenya.
Al-Shabab ambao idadi yao ni kati ya 10 na 15, walivamia jengo hilo na kuteka raia waliokuwemo ndani kisha kuilazimisha Serikali ya Kenya kusalimu amri na kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Kadiri muda ulivyokuwa unasogea mbele, kikundi hicho kilikuwa kinaua raia kwa mafungu, huku kikitishia kuendelea na mauaji zaidi kama Serikali ya Kenya itaendelea kukaidi.
Kila walipoua raia, walimtupa nje ili kutoa ujumbe kwa serikali kwamba dhamira yao ipo hai katika kuilazimisha Kenya kuondoa majeshi yake Somalia.
Mpaka Jumapili jioni, jumla ya watu 59 walikuwa wamesharipotiwa kuuawa katika tukio hilo, huku wengine 175 wakiwa wamejeruhiwa.
“Kipaumbele chetu ni kuokoa watu wengi kadiri tuwezavyo,” Joseph Lenku ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, akihusika na Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali, aliviambia vyombo vya habari.
“Tumeshaokoa takriban watu 1000, tunaendelea na jitihada zaidi,” alisema Lenku.
WAKENYA WAUNGANA
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, mpinzani wake mkuu, Raila Odinga, kwa pamoja walitoa matamko yanayofanana, yakitaka utulivu miongoni mwa raia.
“Kinachotia moyo ni kuona viongozi wote wa Kenya tumesimama pamoja katika kipindi hiki kigumu,” alisema Kenyatta katika mkutano na waandishi wa habari ambao Odinga pia alihudhuria.
Odinga alisema kuwa tukio la Westgate kutekwa siyo vita dhidi ya Waislamu, isipokuwa ni mapambano dhidi ya ugaidi, kauli ambayo Kenyatta aliiunga mkono.

CHANZO: www.globalpublishers.info

HISTORIA YA AL SHABAAB UJUE WALITOKEA WAPI HADI LEO WAMEKUA TISHIO


Kundi la wapiganaji wa kisomali la al-Shabaab,limevamia jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa nchini Kenya. Al Shabaab lenya mizizi yake nchini Somalia, limeweza kuondolewa kutoka miji mikubwa ya Somalia ikiwemo Mogadishu na sehemu zengine za Somalia , ingawa bado linasalia kuwa tisho kubwa kwa kanda nzima.

Al Shabaab ni nani?

Jina Al-Shabab linamaanisha Kijana kwa lugha ya kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa mahakama za kiislmau ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006, wakati ilipopigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini Somalia kuunga mkono serikali iliyokuwa dhaifu. 

Kuna taarifa chungu nzima kuhusu wapiganaji wa kiisilamu wanaokwenda Somalia kupigania Al Shabaab.

Kundi hilo limeweka sheria kali za kiisilamu katika maeneo ambayo linadhibiti ikiwemo kupigwa kwa mawe hadi kufa wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati pamoja na kuwakata wezi mikono.

Je Al Shabaab linadhibiti sehemu gani ya Somalia?

Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti, wa miji mikubwa, bado linakita mizizi katika maeneo ya mashinani.

Lililazimika kuondoka katika mji mkuu Mogadishu, mwezi Agosti mwaka 2011 na pia kuondoka katika mji wa bandarini wa Kismayo mwezi Septemba mwaka 2012.
Kismayo ulikuwa mji muhimu kwa kundi hilo, ambao ulikuwa unawezesha bidhaa kuwafikia wapiganaji wa kundi hilo pamoja na kuwatoza watu ushuru kwa shughuli zao.
Hizi ni silaha za Al Shabaab walizonasa wanajeshi wa AU
Muungano wa Afrika, ambao unaunga mkono juhudi za majeshi ya serikali, ulisherehekea ushindi huo ingawa al-Shabab hunfanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu na kwingineko.
Wadadisi wanaamini kuwa al-Shabab limeanza kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya kushindwa na majeshi ya Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao.
Lakini linakabiliwa na tisho kubwa kutoka kwa wanajeshi wa Kenya walianza hatarakti zao dhidi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2011.
Kenya ilituhumu wapiganaji wa al-Shabab kwa kuwateka nyara wanajeshi wake pamoja na watalii na sasa wamekuwa katika msitari wa mbele kupambana na kundi hilo la kigaidi.
Wakati huo, wanajeshi wa Ethiopia waliweza kukabiliana na wapiganaji hao na kudhibiti miji ya Beledweyne na Baidoa.

Nani kiongozi wa al-Shabab?

Ahmed Abdi Godane ndiye kiongozi wa kundi hilo. Anajulikana kama Mukhtar Abu Zubair, na anatoka katika jimbo la Somaliland.
Kumekuwa na taarifa za mgawanyiko katika kundi hilo, ambazo hata hivyo zinapingwa vikali na kundi lenyewe. Inaarifiwa kuwa uongozi wake unapingwa, na wanachama wanaotoka maeneo ya Kusini na ambao ni wengi katika kundi hilo. Inakisiwa idadi yao ni kati ya wanajeshi 7,000 na 9,000.
Bwana Godane huwa haonekani hadharani . Mtangulizi wake Moalim Aden Hashi Ayro, aliuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani mwaka 2008.

Nini uhusiano wa kimataifa wa kundi hilo?

Al Shabaab wakifanya mashambulizi mjini Mogadishu
Al-Shabab lilijiunga na al-Qaeda mwezi Februari mwaka 2012. Katika ujumbe wa Video, kiongozi wa al-Shabab Ahmed Abdi Godane alisema anaahidi kuunga mkono kingozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri.
Makundi hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi kwa pamoja, na raia wa kigeni wamekuwa wakiunga mkono kundi hilo, na hata kuwasaidia katika harakati zao za mapigano.
Mwaka jana maafisa wa al-Shabab waliambatana na mtu aliyesema ni mwanachama wa al-Qaeda na kumtambua kuwa raia wa Marekani Abu Abdulla Almuhajir alipokuwa anatoa msaada wa chakula kwa waathiriwa wa njaa.
Maafisa nchini Marekani wanaamini kuwa wapiganaji wa Al Qaeeda ambao hawajahusina sana na mashambulizi nchini Afghanistan na Pakistan kufuatia mauaji ya kiongozi wao,Osama bin Laden, wapiganaji wake wengi wanakwenda kutafuta hifadhi nchini Somalia

Hizi ndizo picha zinaonyesha "MAGAIDI" wanavyofanya ugaidi Nairobi Kenya!!!!!























                               Mtu na mchumba wake waliuawa pamoja