Zaidi
ya watu 39 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa baada ya watu wenye
silaha kuliteka jengo lenye maduka la Westgate, jijini Nairobi, Kenya.
Tukio
hilo lilitokea jana mchana ambapo watu waliokuwa wakizungumza lugha ya
kigeni, inayodhaniwa kati ya Kiarabu au Kisomali, kuvamia jengo la
ghorofa na kushambulia watu kwa risasi
“Hawakuwa
wakizungumza Kiswahili. Walikuwa wakizungumza kwa lugha kama vile
Kiarabu au Kisomali, lakini sina hakika sifahamu lugha hizo,” alisema
mmoja wa mashuhuda aliyefanikiwa kutoka ndani ya jengo hilo na
kujitambulisha kwa jina moja la Jay.
Shuhuda
mwingine aliyejitambulisha ni mfanyakazi wa Ubalozi wa Uholanzi jijini
Nairobi, Rob Vandijk, alisema tukio hilo lilitokea wakati akipata
chakula cha mchana ndani ya jengo hilo.
Alisema watu hao waliingia ndani ya jengo la maduka hayo
na kuanza kushambulia watu kwa risasi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Abbas Guled alisema: “Ninachoweza kusema tuna takriban maiti 20. Majeruhi ni wengi.”
Katika
hotuba iliyorushwa moja kwa moja baadaye, Rais Uhuru Kenyatta
alithibitisha kuwa zaidi ya watu 39 walikufa katika shambulizi hilo la
kinyama, na wengine 150 kujeruhiwa.
"Vyombo
vya usalama vinafanya kila jitihada kuthibiti eneo hili na kuwakamata
waliohusika," asema Mr Kenyatta, akiongeza kuwa naye pia amepoteza
wanafamilia katika tukio hilo.
Polisi Waingia
Taarifa zingine zilisema kuwa polisi waliwasili eneo la tukio dakika 30 baada ya watu hao kuvamia jengo hilo.
Kamanda
wa Polisi wa Kenya, Inspekta Jenerali David Kimaiyo alisema kwamba
polisi walifika katika jengo hilo baada ya kupata taarifa, ambapo nao
walianza kujibizana kwa risasi na magaidi hao waliokuwa hapo ndani.
Alisema
watu hao wanaosadikiwa ni magaidi walikuwa wakijaribu kuiba pesa katika
jengo hilo, kabla ya polisi hawajatokea na kuanza kurushiana risasi.
Helikopta za polisi zilionekana zikilizunguka jengo hilo kwa juu kuhakikisha hakuna mhalifu yeyote ambaye anaweza kutoroka.
Mashuhuda
walisema kwamba walikuwa wakipata chakula cha mchana jirani na jengo
hilo, ghafla wakashuhudia milio wa risasi kutoka katika eneo hilo.
Polisi
walifanikiwa kuingia katika jengo hilo baada ya kukaa kwa muda mrefu
kuangalia namna ya kuingia kwa sababu hawakujua watu hao walikuwa
wamejificha eneo gani.
Baada
ya polisi kuingia katika jengo hilo watu waliokuwa ndani walipata fursa
ya kutolewa, huku polisi wengine wakiendelea kuwatafuta wahalifu hao.
Al-Shabab Yanena
Wakati
shambulizi likiendelea jana jioni, wanamgambo wa kikundi cha Kiislamu
cha Al-Shabab walivyambia vyombo vya habari kupitia Twitter kuwa
wamehusika na tukio hilo.
“Tulishaionya serikali ya Kenya kuwa dhahama itaikumba kama isipoondoa vikosi vyake kutoka Somalia,” Al-Shabab waliandika kupitia akaunti yao ya Twitter inayoitwa @HSM_Press.
Wanamgambo hao waliongeza kuwa wamefanikiwa kuua watu wengi ( 100 ) kuliko idadi inayotajwa na serikali ya Kenya, huku wakibeza jitihada za uokoaji.
0 comments:
Post a Comment