MTUHUMIWA,
Manfred Adam anayekabiliwa na kesi ya kutishia kuua katika hali
isiyotarajiwa amelimwaga kojo katika Mahakama ya Mwanzo na kuleta vurugu
kubwa zilizosababisha kuvunjika kwa meza ya Mahakama ya Mwanzo ya
Mazimbu mkoani Morogoro mwanzoni mwa wiki hii.
Katika
vurugu hizo zilizolazimisha shughuli za mahakama kusimama kwa muda wa
saa mbili, askari wawili waliokuwepo eneo la tukio walishindwa
kumdhibiti Manfred, kitendo kilichofanya kuitwa kwa wengine zaidi ambao
waliweza kumtuliza mtuhumiwa huyo.
Hakimu
Alisile Mwankejela aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo namba 322 ya mwaka
2013 pamoja na makarani wa mahakama hiyo walitimua mbio kuhofia
kudhurika, mara tu baada ya vioja hivyo kuanza kufuatia kuahirishwa kwa
kesi ya mtuhumiwa huyo ambayo itasomwa tena Septemba 24, mwaka huu.
“Ni
kweli tukio hilo limetokea baada ya kuhairisha kesi, mshitakiwa huyo
alikojoa mahakamani na kufanya vurugu kubwa,” alisema hakimu huyo
alipokutwa ofisini kwake.
Karani wa makahama hiyo, Kidawa Minangu alimwambia mwandishi wetu;
“Manfed
asubuhi aliletwa hapa kwa ajili ya kesi yake, alipofika tuliita jina
lake na aliingia mahakamani na kusomewa mashitaka yake, kesi
ilipohairishwa cha ajabu alivua suruali na kukojoa hapa mahakamani,
tuliwaita askari wawili wa hapa mahakamani walipomkamata alianza
kupigana nao na kuvunja meza za mahakama ndipo tulipoamua kuomba msaada
wa askari wengine ambao walifika na kumdhibiti
chanzo: audifacejackson.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment