MREMBO
anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo
(pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo
nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika
katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa
Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini,
kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
“Kujiamini
ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu
kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.
“Kujitegemea ni sababu ya
pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama
mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe
unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
Jokate alisema sababu
nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika
mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.
Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
0 comments:
Post a Comment