Sir Andy Chande Mtanzania wa Kwanza kukiri wazi kuwa ni Mwanachama wa Freemason
~ “Nilipoanza kutafuta uanachama
wa Freemason nililazimika kutambua kuwa nilikuwa natumbukia katika
mazingira ambayo sikuwa nayajua, ya kujitenga na dunia.”
~ Asema “Nina hati “takatifu” ya kuhani mkuu freemason”
~ kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ilianzishwa Zanzibar mwaka 1904
Sir Andy Chande ni mtanzania wa kwanza
kukiri kuwa ni mwanachama wa kundi la Freemasons, Chande tofauti na kuwa
member wa kundi hilo pia anakiri kuwa ameshika nyadhifa nyingi ndani ya
kundi hili ikiwa ni pamoja na kutunukiwa hati takatifu ya Kuhani Mkuu.
Katika maelezo yake pia ametaja asasi zilizofadhiliwa na kundi hilo
lililoenea duniani kote.
Maisha yake kama mwanachama wa kundi hilo ameyaweka katika kkitabu chake Katika alichokiita SHUJAA KATIKA AFRIKA, safari kutoka Bukene.
Mzee Chande ni Mtanzania aliyewahi
kushika nyazifa mbali mbali katika utumishi wa umma katika Serikali ya
Tanzania na kujizolea sifa kadhaa ikiwa ni pamoja na Heshima ya “Sir”
aliyopewa na Malkia wa Uingereza.
Katika kitabu hicho ameeleza kwa kina
jinsi alivyoingia katika chama hicho Oktoba 25, mwaka 1954, akianzia na
kambi inayoitwa Jaha iliyomaanisha kundi la watu wa daraja la nne.
Kati ya mwaka 1967 na 2003 Sir Andy
Chande amekuwa mwenyekiti wa Tanzania Tourist Corporation, Tanganyika
Standard Newspapers Ltd, East African Harbours Corporation, East African
Railways Corporation and Cargo Handling Company of East Africa
ltd.Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika mashariki Sir Chande
alikuwa mwenyekiti wa Air Tanzania Corporation na baadaye akafanya kazi
kama Mwenyekiti Mamlaka ya Bandari Tanzania na pia Mwenyekiti wa
Tanzania Railways Corporation.
Katika Ukurasa wa 168 wa kitabu hiki
kilichozinduliwa kwa heshima na viongozi wa wakuu wa serikali ya
Tanzania, Sir Chande anasema:
Jengo la Freemasons lililoko
maeneo ya Posta jijini Dar es salaam
|
“Kuwa mwanachama wa Freemason maana
yake ni mtu kujitolea kuingia katika safari ndefu isiyo na mwisho ya
kujifunza na kuchunguza. Kwa muda wa miaka 50 iliyopita mafunzo yangu
ndani ya Freemason yaniwezesha kupata shahada nyingi za ngazi na umuhimu
unaozidiana, ukiacha ukuu wa Wilaya nzima ya Afrika Mashariki, yaani
Kenya Sheli Sheli, Tanzania na Uganda, kwa miaka 19. Nikitaja nafasi
chache tu nilizoshika, nimekuwa msimamizi wa kwanza mdogo kasha mkubwa
wa kambi kuu ya viongozi wa Freemasons wa Uingereza na Wiles.
Mara ya kwanza kabisa nafasi hiyo
kushikwa na mtu asiye mkazi wa Uingereza. Nimepewa heshima ya kuwa
mstahiki kamanda wa kambi ya Donyo sabuki ya royal Ark Mariner na
nimeshika uongozi wa kambi hiyo toka mwaka 1990.
Mimi ni msimamizi mkuu wa Afrika mashariki wa kikosi kikuu cha Freemason cha Royal Ark cha Uingereza,
nikiwa nimeshika nafasi hiyo tangu mwaka 1980, na ofisi ya wilaya tangu
mwaka 1972. Mwaka 2000 nikawa Naibu Mshika upanga mkuu wa kikosi kikuu,
na bado mimi ni mkufunzi mkuu wa heshma katika kikosi kikuu cha
Uskochi.
Mwaka 1987 nilipata shahada ya
Mtakatifu Lawrence, shahidi; Shada ya shujaa wa Constantinople hati
takatifu ya Kuhani Mkuu na Wawekezaji wakuu wa Suleiman; nikapata
vilevile hati muhimu ya ushujaa ya msalaba mwekundu wa babeli mwaka
1988, nikaingia katika halmashauri ya wasimazimi wakuu namba 1,
walioteuliwa na waliokuwa hodari mno nchini Uingereza na Wales, na
nikapewa shahada ya msimamizi bora kuliko wengine wote. Mwaka uliofuata nikaingia kama mwanafunzi wa mkataba katika jamii ya waabudu wa Freemasons, tawi la Row Assemblege”.
Katika maelezo ya Sir Chande hapo juu
kama yaliyonukuliwa katika kitabu chake hicho chenye kuheshimiwa sana
nchini napengine hata duniani, yapo mambo mawili yenye kuhitaji
udadavuzi makini zaidi. Mambo hayo ni mafunzo ya matambiko na jamii ya
waabudu wa Freemasons.
Hata hivyo katika maelezo ya awali Sir
Chande anasema chama hicho sio dini na wala hakiingilii dini ya mtu,
wala hakimkatazi mwanachama wake kuabudu dini nyingine.
Uchunguzi wa Mpekuziblog umebaini
kuwa chapisho la Kiswahili la kitabu hicho lilizinduliwa katika hafla
kubwa iliyohudhuriwa na viongozi wakuu wanchi marais wastafu, mabalozi
na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, katika ukumbi wa shule
ya Sekondari ya Shaaban Robert, Agosti 10, mwaka 2007.
BAADHI YA MANENO YA HOTUBA YA JK
Maneno yaliyopo kwenye hotuba ya Rais kikwete wakati wa uzinduzi wa kitabu hiki yanadhihirisha
upekee na umuhimu wake na hata kile kilichomo ambacho wengi hawakijui.
Rais katika sehemu ya hotuba hiyo alisema:
“….Aidha, napenda kukupongeza kwa
dhati kwa kitendo chako cha kuandika kitabu hiki kinachohusu maisha
yako. Sote tunatambua kuwa kuandika kitabu sio kazi rahisi hata kidogo.
Ni jambo linalohitaji ujasiri, umakini, nidhamu na uwezo wa hali ya
juu. Hivyo kwa kuandika kitabu hiki kinachogusia maisha yako kwa
kipindi kinachozidi miaka 77 umeonyesha wazi kipaji na uwezo mkubwa ulio
nao. Si watu wengi walio na uwezo kama ulionao wewe. Tunakupongeza
sana.
Lakini kubwa zaidi nakupongeza kwa
kuandika kitabu hiki kwa umakini na ufasaha mkubwa. Umeweza kwa kiwango
cha hali ya juu kueleza mazingira halisi ya hali ya nchi yetu
ulimokulia, kufanyia kazi na sasa unamozeekea. Kitabu chako ni mchango
mkubwa kwa historia ya nchi yetu ambayo tunauenzi kwa faida ya kizazi
cha sasa na kijacho.
Nawaomba watanzania wenzangu
wakisome kitabu hiki kila watakapopata nafasi, ninahakika watafaidika
sana na kile watakachokisoma. Ingekuwa jambo jema sana maktaba za shule
na vyuo vyetu vikawa na nakala ya kitabu hiki, hivyo kuwawezesha vijana
wetu kufahamu kwa undani zaidi historia ya nchi yetu na watu wake kwa
ujumla”
Rais Kikwete akiwa na kiongozi
mkuu wa mafreemason ,Sir Andy Chande
|
Lakini hofu kubwa kwa jamii
isiyofahamu vyema mambo hayo ni kuwepo kwa neno kuabudu ambalo tafsiri
rahisi ni Tafsiri hahisi ya Neno Matambiko lililopo katika maelezo
binafsi ya Sir Chande. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu ni:
Utekelezaji wa ada maalumu ili kutuliza mizimu, au pepo, edah, kafara,
mviga mviko.
Tafsiri ya Neno kuabudu ni: “kufanya
ibada, kuheshimu kwa hali ya juu unyenyekevu wa hali ya ju. Aidha
tafsiri nyingine zaidi ni tendo linaloambatana na kutoa sadaka.
Akieleza safari yake jinsi alivyojiunga na kundi hilo Sir Chande alisema.
“Nilipoanza kutafuta uanachama wa
Freemason nililazimika kutambu kuwa nilikuwa natumbukia katika mazingira
ambayo sikuwa nayajua, ya kujitenga na dunia. Maana ingawa mpaka wakati
huo Chama cha Freemason kilikuwa katika sura hiyo hiyo kwa karibu miaka
mia tatu (Kambi hizo mbili ziliunganishwa uingereza mwaka 1715), hali
ya usirisiri wake unaokigubika imeongezeka sana katika miaka hii
michache.
Freemason walikuwako katika sehemu
yangu hii ya dunia kwa muda wa miaka hamsini, kambi ya kwanza ya Afrika
Mashariki ikiwa imeanzishwa Zanzibar mwaka 1904, lakini ikichukua miaka
mingine ishirini na minne kwa kambi ya kwanza ambayo, kwa shamra nyingi,
Gavana ndiye aliyeiwekea jiwe la msingi ili ijengwe huko Bara katika
Mtaa ulioitwa wakati ule; Main Avenue, sasa hivi Sokoine.
chanzo: calvin-obeld-blog.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment