IMEVUJA!
Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na
filamu za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ na shosti wake, Mellisa
Edward kabla ya kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya
‘unga’ Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili
kutaja waliowatuma.
Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.
Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.
Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.
Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.
MATESO SAA 24
Chanzo hicho
kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao
wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema
aliyewatuma.
USHUHUDA
“Unajua
Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya.
Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.
“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.
“Kwanza utaanzia kwenye chumba
kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi
ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani
hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.
“Wakishakuingiza mle ndipo
utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima,
zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.
“Kama bado ukijifanya mbishi
au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja
ndogo kwenye waya wa umeme.
“Si unajua tena waya wenye
umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya
kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.
“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.
“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.
WALIOWATUMA
“Baada
ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya
crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,”
kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa
wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi
kukumbwa na mkasa kama huo.
MTOTO WA KIGOGO ATAJWA
Habari
za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao
waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni
mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina
lipo).
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa
mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha
mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni,
mwaka huu.
Ilivuja kuwa mwingine
aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo
anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga
likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George
Mwakyembe.
Gazeti hili lilipozungumza na
Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey
Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili
kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.
ULINZI MKALI
Baada
ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na
maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti
19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali
WAPANDISHWA TENA KORTINI
Habari
kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena
kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma
ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si
chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.
Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHER BLOG
0 comments:
Post a Comment