DJ FETTY KTK MASHINE.
Nikitaja majina ya Watangazaji na Madj’s ambao ni kipenzi cha
mashabiki wengi wa muziki walioko kwenye chat kwa hapa nchini ni lazima
utakutana na jina ‘Fetty’ hautalikosa katika ukurasa wowote wa burudani.
Binti
huyu ni shombeshombe wa kisomali aliyezaliwa Mkoani Shinyanga miaka
fulani ya themanini japo si mksukuma.Baadaye akaingia jiji la Dar es
Salaam ambapo alipata elimu yake yote ya sekondari.
‘Fetty’
anasema mwaka 2003 alivutia sana Babra Hassan wakati huo akitangaza
kipindi cha ‘Hang out’ saa sita mpaka saa nane mchana kituo hicho cha
Clouds Fm.
“Kiukweli alikuwa alinishawishi sana Safari ya kutimiza
ndoto zangu za utangazaji, sikuwa nimesomea kazi hii lakini niliamini
kuwa nitaweza mwaka wa 2004 nilienda ofisi za Clouds,niliomba kutangaza
lakini haikuwa rahisi baadaye nilianza kuingia studio kumsikiliza Babla
anavyotangaza”anasema Fety.
Kuanza kutangaza
Fetty anasema baada ya Babla
kuacha kazi mwishoni mwa mwaka 2004 akitangaza kipindi hicho
alikabidhiwa kukiendesha ndani ya masaa 3,bila kuongea hewani baadaye
aliamua kuongea na Dj Nelly amfundishe kazi ya kuchezea sahani za
muziki,alionekana kufanya vizuri na ilipofika mwaka 2006 mambo yakawa
safi.
“Nikaanza kusikika kidogo kidogo kwenye kipindi cha nyuki
Dj’s ambapo kulikuwa na Jamaa sita na mtoto wa kike peke yangu,kipindi
hicho kilikuwa siku ya Jumamosi ndani ya masaa 3 na nusu,ilipoanza julai
2006 tulianza kusikika mimi na ‘Muli B’
Anasema baada ya kufanya
vizuri alipewa ofa ya kwenda Uingereza kusoma kozi fupi ya Utangazaji na
alifanikiwa kurudi na wazo jipya la kipindi alichokiita ‘soso fresh’
kilicho maanisha kila kitu sawa ambacho kilifanya vizuri zaidi.
“Kipindi
hicho nilikifanya kwa mwaka mmoja baadaye mabosi wakaona nafanya vizuri
wakanipa majaribio ya miezi mitatu kipindi kikubwa cha ‘Top 20’
nikafanya vizuri,mashabiki walinikubali sana baadaye wakaona ‘bongo
fleva’ inapwaya ambayo niliendelea nayo mpaka sasa.
Mafanikio yako
“Nia
ya kuamua kufanya jambo fulani,Tamasha la Fiesta limenitoa sana
ukiachana na kazi ya utangazaji japo ndio kazi iliyonijengea kwa mambo
mengi,Tamasha la Fiesta ndio limefanya watu kunikubali zaidi,walikuwa
wanamsikia fet kwenye Radio kwa hiyo wanaposikia tamasha wanatamani
kumuona.nafasi ya Dj’s ni zaidi ya utangazaji kwangu.
Fetty
anasema kupitia kazi ya utangazaji na Dj imemletea mafanikio ya kuwa na
kampuni inayojulikana kwa jina la ‘fettylious’ inayohusika na matangazo
na kutengezesha nembo za tishet.kwa hiyo anasema maisha yake ni mazuri
kwa sababu anapata anachokita.
Ndoto zako
Tukiachana
na tukio la kushangiliwa jumba la ‘Big Brother’ Fetty bado
anatamani siku moja aweze kusikika kwenye Vituo vya Radio za kimataifa
kama vile BBC na Aljazir,mbali na ndoto hizo anamshukuru Mungu kwa
nafasi aliyonayo kwa sasa kwani ametokea kuwa kipenzi cha watanzania
wengi wanaopenda Muziki.
“Tukio la Dodoma miaka 10 ya fiesta
nilishangaa watu walivyonipokea,walinitia moyo na kuamini kuwa
ninapendwa yaani maelfu walitamani kunishika hata mkono lakini
kilichosaidia ni askari.
Maisha yako na Jamii
“Yako
poa sana ninaweza kujichanya na jamii yoyote hata tandale
naishi,sipendi mtu anayefanikiwa na kusahau alikotokea kwa mfano unaenda
Marekani miaka mitatu unarudi yes,no zinakuwa nyingi,unajifanya hujui
tena kiswahili.
Fetty anasema yeye anaweza kuongea lugha ya kisukuma vizuri tu japo sio lugha yake pamoja kuishi mjini kwa mda mrefu.
Chakula anachopenda
“Hata
kama nipo usingizini ukiniamsha usiku wa manane kama nina njaa
nitakuomba Wali na Maharagwe ,ni chakula ambacho kwa kweli ninakipenda
sana kelvin.
Una mchumba
“Da swali hilo kila
mtu huwa anapenda kuniuliza lakini huwa sipendi kueleza chochote juu ya
mahusiano yangu,wanaosema nina mtoto wa kigogo sio kweli maisha yangu
yasingekuwa haya pengine ningekuwa namiliki Benzi au Vog’,sitaki kuweka
wazi juu ya hilo.
Ila Fetty anapaza sauti mwanaume ambaye anaweza
kuishi nae akisema ni yule ambaye ataweza kutoa ushirikiano katika kazi
za ndani,anayemjali na kumthamini.
Tanzania ya kesho
“Natamani sana kuona serikali
inafanikiwa kuondoa changamoto ya foleni, yaani msongamano wa magari
imekuwa kero kubwa inakwamisha mambo mengi,ufisadi unaongezeka wanakula
pesa zetu kila kukicha,natamani kupata kiongozi atakaye maliza kero
hizi.
Chanzo Gazeti la Mwananchi
0 comments:
Post a Comment