AMA kweli hii bombastiki! Daktari
Afrika Kweka amenaswa katika Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ akiwa katika
jaribio la kumtoa mimba mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Stella.
Awali, raia wema wa eneo hilo walituma malalamiko yao kwa OFM wakidai kwamba, Dokta Kweka amekuwa akifanya ‘mauaji’ hayo ya vichanga waziwazi, hali inayowakera kupita maelezo.
Baada ya kupata taarifa hiyo, OFM ilipanga mtego ambapo mmoja wa waandishi wetu wa kike alikwenda kwa Dokta Kweka na kujifanya mwanafunzi wa chuo lakini ana mimba anataka kuichoropoa.
Dk. Kweka.
Mwandishi huyo aliingia na
paparazi wa kiume aliyejifanya ni mpenzi wake aliyempa mimba hiyo. Ndani
ya eneo la tukio walipokelewa kwa bashasha na daktari huyo ambaye
alihitaji shilingi 60,000 kama gharama za kutoa mimba japo baadaye
alikubali kushusha bei hadi shilingi 45,000.
Baadaye daktari huyo alimchukua
mwandishi wetu bila kujua kama hakuwa na mimba wala kitambi na kumpeleka
chumba cha kuchomea sindano ambapo almanusura mpango mzima uharibike
kwa kuwa mwandishi wetu hakupaswa kuruhusu daktari huyo amchome sindano
ambayo ilisadikika kuwa ni ya ganzi.
Hata
hivyo, wakati paparazi wetu akijishauri kuhusu sindano hiyo, ndipo
Stella alifika kwenye zahanati hiyo na kuingia ndani kwa dhumuni la
kutoa mimba.
Alipofika aliingia moja kwa moja chumbani kwa daktari huyo na kuchoma sindano ya ganzi bila woga kisha akaingia chumba cha kuchoropolea.
Alipofika aliingia moja kwa moja chumbani kwa daktari huyo na kuchoma sindano ya ganzi bila woga kisha akaingia chumba cha kuchoropolea.
OFM ilipata uhakika kuwa,
mwanamke huyo ameingia chumba cha kutolea mimba, ndipo ‘wapenzi’ hao
(mapaparazi wetu) waliwasiliana na wapiga picha wetu waliokuwa chobingo
na polisi ambao walitia timu na kuwanasa.
Daktari huyo na mteja wake walipelekwa kituo cha polisi na kufunguliwa jalada la kesi namba MMP/RB/567/2013 kosa likiwa kujaribu kutoa mimba huku ikibainika kuwa zahanati hiyo ni batili kwa kuwa aliisajili kama maabara.
Daktari huyo na mteja wake walipelekwa kituo cha polisi na kufunguliwa jalada la kesi namba MMP/RB/567/2013 kosa likiwa kujaribu kutoa mimba huku ikibainika kuwa zahanati hiyo ni batili kwa kuwa aliisajili kama maabara.
“Mbaya zaidi huyu jamaa amekuwa akitumia risiti za CCM katika mambo yake, lazima aondoke kwa kweli, tunamwandikia barua.”
Imeandaliwa na Chande Abdallah, Denis Mtima, Mayasa Mariwata, Issa Mnally, Richard Bukos na Hamida Hassan.
0 comments:
Post a Comment